Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bajeti 2019/20: Ushabiki wa kisiasa wateka Bunge
Habari za SiasaTangulizi

Bajeti 2019/20: Ushabiki wa kisiasa wateka Bunge

Spread the love

TOFAUTI na bajeti za serikali katika miaka ya fedha iliyopita, katika Mwaka wa Fedha wa 2019/20, ushabiki wa kisiasa umedhihiri. Anaripoti Dandon Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ushabiki huo ulikomaa baada ya Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango, kutaja sifa 10 za wagombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa Oktoba mwaka huu, baada ya kutaja sifa za wagombea hao.

Wakati Dk. Mpango akitaja sifa hizo leo tarehe 13 Juni 2019 bungeni jijini Dodoma, wabunge waliibua kelele ambazo zilisababisha waziri huo kushindwa kuendelea kusoma bajeti hiyo.

Job Ndugai, Spika wa Bunge aliingilia kati kutuliza kelele hizo zilizokuwa zikitoka kwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliokuwa wakiimba ‘CCM’ ‘CCM’ ‘CCM.’

Pamoja na Spika Ndugai kutuliza kelele hizo zilizotoka kwa wabunge wa CCM, wabunge hao waliendelea hivyo Spika Ndugai kutumbukia humo na kumtaka Dk. Mpango kurudia kipengele cha 10 cha sifa hizo.

Dk. Mpango kwa ombo la Spika Ndugai, alirudia kipengele hicho huku akihitisha kwa kusema kuwa, wagombea wenye sifa hizo wanatoka CCM.

Akisoma Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 jijini Dodoma leo tarehe 13 Juni 2019, ambapo serikali imeomba Sh. 33.11 trilioni, Dk. Mpango amesema, serikali imejiandaa kuingia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Dk. Mpango aliwataka wananchi kuchagua watu wenye sifa za kuwaongoza, akitaja sifa hizo alisema ni pamoja na:-

Kwanza: Awe mchapakazi mwenye kujitoa sadaka kuwatumikia watu hasa wananchi wa kawaida.

Pili: Awe mwepesi kuona, kusikiliza na kuguswa na shida za wananchi wake, tena awe jasiri katika kupigania haki za wanyonge na awe na uwezo na ubunifu wa kutatua kero za wananchi hao.

Tatu: Awe mwadilifu anayechukia na kupiga vita rushwa na ufisadi kwa vitendo.

Nne: Anayetambua fursa zilizopo katika eneo lake, kubuni mikakati ya kuwaendeleza wananchi anaowaongaza na kuwatia watu wake hamasa ya kuthubutu kutumia fursa hizo.

Tano: Awe mtetezi hodari wa kulinda mazingira na awe mpambanaji hodari zidi ya athari  za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Sita: Sita awe haabudu nyazifa, anayetambua kuwa nafasi na vyeo tulivyopewa ni vya muda tu, thamani halisi ya kiongozi ni kuacha kumbukumbu mzuri kwa ustawi wa eneo analoliongoza na kwa taifa kwa ujumla.

Saba: Awe kama mchezaji mzuri wa kiungo katika timu ya ushindi anayetambua kwamba, mkono mmoja hauwezi kupiga makofi ya shangwe.

Nane: Awe mwenyekutambua ya kwamba, kazi za kiongozi zinamaana sana kwa kuwa, zinaweza kubadilisha maisha ya maelfu ya Watanzania na hasa wanyonge kuwa bora zaidi.

Tisa: Awe na uwezo wa kueleza wananchi kinaganga kuhusu serikali yao, na inawapeleka wapi kwa kila mmoja ili waendelee kuiunga mkono.

10: Awe anatoka ndani ya chama cha siasa. Na chama hicho ni CCM

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!