Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango na bajeti isiyotekelezeka
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango na bajeti isiyotekelezeka

Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango akionesha begi lenye Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2019/20
Spread the love

BAJETI ya serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20, iliyosomwa na Dk. Philiph Mpango, waziri wa fedha na mipango, katika utawala wa Rais John Pombe Magufuli, haina jipya. Imejirudia mambo yale yam waka uliyopita; na au miaka mitatu ya nyuma. Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).

Mathalani, ndani ya bajeti hakuna nyongeza ya mishahara. Siyo tu, kwamba mishahara haikuongezwa, bali pia serikali imeshindwa kuondoa; na au kuondoa kodi kwenye mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya umma.

Bajeti haikuzungumzia kuhusu uzalishaji kwenye viwanda na kilimo. Badala yake, bajeti imeishia kupanga mikakati ya ukusanyaji kodi.

Bajeti haikuzungumzia kodi kwenye mafuta yanayotumika katika sekta ya madini. Kwa mfano, makampuni ya madini, pamoja na kuvuna faida kubwa, hawalipi kodi ya mafuta wanayotumia na mara ya mwisho ilipendekezwa waanze kulipa.

Migodi mingi inapata faida kubwa na inapanuka kibiashara; na sasa wako kwenye soko la dhahabu la dunia, lakini serikali imekiacha chanzo hiki na kuishia kuanzisha kodi mpya kwenye nywele za bandia, biskuti, pipi ubani na soseji. 

Kwa miaka mingi, makampuni ya uchimbaji madini nchini, imekuwa ikipewa na serikali misamaha ya kodi.

Serikali yenye kujali wananchi wake, ilitarajiwa iliangalie suala hilo kwa makini na si kuwaomba, bali kuwaelekeza tu kwamba ile kodi ambayo hawakuwa wakilipa, sasa waanze kulipa kwa kuwa hali ya uchumi siyo nzuri.

Kama serikali ikichukua mkondo huo, inaweza kupata dola 250 milioni ambazo wafadhili wamepunguza.

Serikali makini ilitarajiwa kukabiliana na hali hiyo kwanza, kabla ya kukurupuka na kuanzisha vyanzo vipya vya kodi. Ilitarajiwa wananchi wasikie mipango ya serikali ya kuimarisha kwa vitendo bandari za Tanga, Mtwara na Kigoma ili kuongeza mapato.

Bajeti haikuzungumzia maswala ya msingi kama uwekezaji katika sekta zinazogusa watu na zenye matokeo makubwa kwa haraka kama uvuvi, kilimo na mifugo. Imeishia kwenye uwekezaji ule wa miaka nenda rudi.

Katika mwaka wa fedha unaoishia Juni mwaka huu, serikali haijatoa hata shilingi kwenye sekta ya umwagiliaji. 

Hata kwenye maji, serikali imetoa chini ya asilimia 17, huku kilimo ambacho ndio uti wa mgongo wa serikali ya Magufuli, hadi Aprili mwaka huu, serikali imetoa chini ya asilimia 42.

Kwenye sekta ya viwanda ambako ndiko kwenye kauli mbiu ya serikali ya taifa la viwanda, kumetolewa chini ya asilimia 32; jambo ambalo litasababisha kuendelea kuagiza chakula kutoka nje – sukari, mafuta na mchele.

Bajeti imeondoa kodi kwenye ngano inayoagizwa nje; lakini imerudisha kwa kasi kodi kwenye pedi za kike. Serikali imeamua kuchukua hatua hizi bila kuangalia hali za wananchi wake. Hakuna ubishi kwamba hali za wananchi hivi sasa zimekuwa duni, ikilinganishwa na kabla ya Magufuli kuingia madarakani.

Katika maingira hayo, kama haya ndio mapendekezo ya serikali kwa

Hata bei za mafuta – petroli, dizeli, mafuta ya taa na yale kupikia – hatabaki salama katika mazingira haya ya kukukusanya na kukusanya kila uchwao.

Bajeti ya Dk. Mpango haina kipya. Ni bajeti iliyoandaliwa kisiasa, iliyojaa mipango isiyotekelezeka na inayojikanganya kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!