Anna Mgwira kumrithi Meck Sadick – MwanaHALISI Online
Anna Mgwira, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Anna Mgwira, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Anna Mgwira kumrithi Meck Sadick

JOHN Magufuli, Rais wa Tanzania amemteua Anna Mgwira, Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo kuwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, anaandika Hamisi Mguta.

Mgwira ambaye alikuwa mmoja wa wapinzani wa Rais Magufuli katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 anachukua nafasi hiyo iliyoachwa na Said Meck Sadick aliyekuwa mkuu wa mkoa huo ambaye alijiuzulu nafasi hiyo.

Wakati huo huo, Rais amemteua Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor aliyekuwa Mkuu wa Oparesheni ya Mafunzo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuwa balozi.

Pia amemteua DIGP Abdulrahman Kaniki aliyekuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi kuwa balozi. Hata hivyo tarehe ya kuapishwa kwao bado haijatangazwa rasmi.

JOHN Magufuli, Rais wa Tanzania amemteua Anna Mgwira, Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo kuwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, anaandika Hamisi Mguta. Mgwira ambaye alikuwa mmoja wa wapinzani wa Rais Magufuli katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 anachukua nafasi hiyo iliyoachwa na Said Meck Sadick aliyekuwa mkuu wa mkoa huo ambaye alijiuzulu nafasi hiyo. Wakati huo huo, Rais amemteua Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor aliyekuwa Mkuu wa Oparesheni ya Mafunzo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuwa balozi. Pia amemteua DIGP Abdulrahman Kaniki aliyekuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi kuwa balozi. Hata hivyo tarehe ya kuapishwa kwao bado haijatangazwa rasmi.

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Hamisi Mguta

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube