August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bulaya, Mdee wazuiwa kuingia bungeni mpaka mwakani

Wabunge Ester Bulaya na Halima Mdee

Spread the love

BUNGE la Tanzania limetoa hukumu kwa Wabunge Halima Mdee wa Kawe na Esther Bulaya wa Bunda kutohudhuria vikao vyote vya bunge vinavyoendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19, anaandika Hamisi Mguta.

Kamati ya Maadili  leo imesema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge, huku hukumu hiyo ikiungwa mkono na wabunge wengi.

Hata hivyo, Bunge liliendelea  kujadili makosa ya wabunge hao huku George Mkuchika, Mwenyekiti wa kamati hiyo akiomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao.

Kanuni inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.

 

error: Content is protected !!