Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto aweka hadharani sababu 10 za kuing’oa CCM 2020
Habari za SiasaTangulizi

Zitto aweka hadharani sababu 10 za kuing’oa CCM 2020

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ameeleza sababu 10 za kuking’oa Chama cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea). 

Zitto ametaja sababu hizo wakati akifungua mkutano mkuu wa chama hicho,  leo tarehe 14 Machi 2020, jijini Dar es Salaam, Zitto

Miongoni mwa sababu alizotaja Zitto ni, CCM kupasuka kutokana na kundi kubwa la chama hicho, kuchoshwa na vitendo vya ubabe, huku nyingine ikiwa ni mdororo wa uchumi wa taifa na wa wananchi.

“CCM imo vipande vipande, kundi kubwa limechoshwa na ubabe. Katika kipindi cha udikteta, CCM imeshaharibu uchumi wa nchi, imefukarisha wananchi. CCM haipaswi kukaa madarakani hata kwa mwezi mmoja,” amedai Zitto.

Sababu nyingine alizotaja Zitto ni, CCM kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi, pamoja na kukosa mbinu za kuwakwamua wananchi katika ufukara.

“CCM chama laghai, hakitimizi ahadi zake, Watanzania hawawezi kukubali kufanywa watoto wadogo. Pia, imeshiwa mbinu na maarifa katika kukwamua Watanzania kwenye umasikini,” amesema Zitto.

Pia, Zitto amesema kudorola kwa sekta ya elimu kutokana na utekelezaji wa sera mbovu, kutasaidia ACT-Wazalendo kuiangusha CCM katika uchaguzi ujao.

“Utekelezaji sera elimu bure umeanza kubainika umetoa elimu bure.  Elimu inazidi kuporomoka, wanafunzi walioahidiwa mikopo wanafukuzwa kwa kudai mikopo,” amesema Zitto.

Sababu nyingine alizotaja Zitto ni “CCM haina mkakati wa kutatua changamoto ya ajira,  kupitia sera mbovu za CCM maisha ya Watanzania yamekuwa magumu, hifadhi ya chakula inatosha kwa siku mbili.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!