April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tendai Biti kuhutubia mkutano mkuu ACT-Wazalendo

Tendai Biti, Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Zimbabwe

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kinachotimiza miaka mitano tangu kuanzishwa, leo tarehe 14 Machi 2020 kinaanza mkutano wake mkuu wa pili kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, utakaohusisha pia uchaguzi wa viongozi wake wakuu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, amesema katika taarifa aliyoitoa jana tarehe 13 Machi 2020 mara baada ya mdahalo wa wagombea wa nafasi ya ukuu wa chama na mwenyekiti, kuwa katika siku ya ufunguzi, wajumbe watasikiliza hotuba za viongozi wa kitaifa na kimataifa walioalikwa, wakiwemo wageni kutoka nje ya nchi.

Amesema wageni hao watakuwa ni wanasiasa kutoka vyama rafiki vya siasa vya Tanzania na nje pamoja na wanadiplomasia wa mataifa na taasisi mbalimbali za kidemokrasia na haki za binadamu.

Hotuba kuu itakuwa ni ya Kiongozi Mkuu wa Chama, Zitto Zuberi Kabwe akitarajiwa kuelezea hatua zilizofikiwa za kuijenga ACT-Wazalendo, hali ya sasa ya nchi kisiasa na kiuchumi, kwa kuzingatia mwenendo wa siasa Tanzania, taifa ambalo litaendesha uchaguzi mkuu mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya uenezi, Tendai Biti, Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe, ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya ufunguzi wa mkutano huo. Biti ni Makamu wa Rais wa Chama cha Movement for Demomcratic Change (MDC) cha Zimbabwe, kilichoasisiwa na Morgan Tsvangirai, aliyekuwa mpinzani mkuu wa Robert Mugabe ambaye baada ya kufanikisha harakati za uhuru mwaka 1980, aliiongoza nchi hiyo mpaka alipoondolewa madarakani kwa ushawishi wa jeshi mwaka juzi. Tsvangirai alifariki dunia mwaka 2018 wakati Mugabe alifariki Septemba mwaka jana.

Ado amesema katika mkutano huo, agenda nyingine kuu mbali na uchaguzi wa viongozi wakuu, itakuwa ni ya mabadiliko ya katiba ya chama, kulingana na hali ya nchi hasa ikizingatiwa kuwa uendeshaji wa siasa nchini umebadilika baada ya Sheria ya Vyama vya Siasa nchini kufanyiwa marekebisho makubwa yaliyompa Msajili wa Vyama vya Siasa, madaraka makubwa katika utaratibu wa kuvisimamia vyama.

“Mkutano ni fursa ya kujadili na kufanya maamuzi juu ya masuala mbalimbali ndani ya chama na kitaifa. Utabeba mambo yote. Kutakua na mambo makuu mawili. Kwanza mkutano mkuu wa uchaguzi, tutatumia fursa hii ya siku tatu kukamilisha safu ya viongozi wa kitaifa wa chama chetu. Tutachagua Mwenyekiti, makamu, kiongozi mkuu wa chama na wajumbe halmashauri kuu ya taifa,” amesema Ado.

error: Content is protected !!