SHIRIKA la Bima Zanzibar (ZIC) limewakaribisha wawekezaji Visiwani Zanzibar kuwekeza kwa kuwahakikishia usalama wa uwekezaji na mali zao wakati wote wakiwepo Visiwani humo. Anaripoti Matilda Buguye, Zanzibar … (endelea).
Hayo yameelezwa jana tarehe 25 Februari, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la (ZIC), Arafat Haji katika maonesho ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Falme za Kiarabu-Dubai.
Haji amewakaribisha wadau kuwekeza Visiwani Zanzibar na kupitia Shirika hilo kwani wana uzoefu na masuala ya bima za aina mbalimbali.
“Wawekezaji tunawapa elimu ya namna gani wataweza kuwa na uwekezaji wenye usalama na kuhakikisha kunakua na ajira ya muda mrefu ili kuleta tija na kukuza uchumi na maslahi ya Taifa,” amesema.
Aidha, Haji ameeleza kuwa wawekezaji wanapoamua kushirikisha ZIC wanafanya maamuzi sahihi kwani wapo tayari kuwapa miongozo ya kusimamia uwekezaji huo na kuhakikisha mitaji yao inaleta manufaa.
Leave a comment