Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari Yanga kusaka pointi 35 za Ubingwa
HabariMichezo

Yanga kusaka pointi 35 za Ubingwa

Spread the love

 

UONGOZI wa klabu ya Soka ya Yanga umesema kuwa, katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanahitaji pointi 35 tu, ili kuwa mabingwa wa wapya wa msimu wa 2021/22. Anaripoti Kelvin Mwaipungu

Yanga wanakwenda kuanza duru la pili kesho tarehe 27 Februari 2022, dhidi ya Kagera Sugar mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam majira ya saa 1 usiku.

Akizungumza kwenye kipindi cha kurasa za magazeti kinachorushwa hewani na televisheni ya Azam, Afisa Habari wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli alifunguka kuwa mahesabu yao kwa sasa ni kutafuta alama hizo katika michezo 15 iliyosalia.

“Sasa tunakwenda kwenye duru la pili ambalo linapointi 45, kiuhalisia sisi tukipata pointi 35 tu, sisi ni mabingwa bila kujali wengine wamefanya nini?.” Alisema Bumbuli

Katika mzunguko wa kwanza wa Ligi uliomalizika hivi karibuni, Yanga walicheza michezo 15 bila kupoteza mechi yoyote huku akivuna jumla ya pointi 39 katika 45.

Aidha Afisa Habari huyo aliendelea kwa kuwataka wanayanga kuendelea kuwa kitu kimoja, kwenye zoezi hilo la kukusanya alama hizo 35 katika duru hilo la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Wanayanga tuwe pamoja kwenye zoezi hili, leo jioni kwenye mazoezi AVIC Town, uongozi wa klabu ya Yanga kamati ya mashindano tutakutana na timu kuzungumza nao.”

Katika kampeni hiyo ya kukusanya alama 35, Yanga itaanza kwa kushuka dimbani siku ya kesho kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambapo kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Kaitaba, Yanga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0.

Kuelekea mchezo huo, Bumbuli alisema kuwa, wapinzani wao kwenye mchezo huo wamekuwa na rekodi ya kuwasumbua kwenye dimba la Mkapa na hivyo wameshapata tiba yao.

“Tunanaza kesho na Kagera wamekuwa na rekodi za kutusumbua hapa na sio kwao, keshjo tunaaenda kutibu kile ambacho kilitutokea misimu mitatu iliyopita.”

“Kesho twende tukalianzishe gurudumu letu la kusaka pointi 35 za ubingwa” alisema Afisa habari huyo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!