Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari Pablo aimaliza Berkane, awapa maagizo maalumu wachezaji
HabariMichezo

Pablo aimaliza Berkane, awapa maagizo maalumu wachezaji

Spread the love

 

NI kama swala la muda tu kikosi cha klabu ya Soimba kushuka dimbani kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya RS Berkane ya nchini Morocco, wachezaji wa klabu hiyo wakijinasibu kuondoka na ushindi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezop huo wa kundi D, utapigwa kesho Jumapili Februari 27 mwaka huu, ambapo utakuwa mchezo wa tatu kwa Simba toka walipoanza kampeni hiyo.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari wakiwa nchini Moroco mchezaji mwandamizi wa klabu hiyo, Erasto Nyoni amefunguka kuwa, tayari wamwshajiandaa kwa ajili ya mchezo huo mara baada ya kocha wao mkuu Pablo Franco Martini kuwapa maelekezo.

“Kikubwa sisi tumejiandaa kimwili na kiakili, tunajianda kufanya kile mwalimu alichotuelekeza ndani ya uwanja, ili kuhakikisha tunaweza kupata matokeo katika mchezo unaofuata.” Alisema Erasto

Simba wanaingia katika mchezo huo wa duru la tatu huku wakiwa kileleni kwenye msimamo wa kundi D, wakiwa na alama nne mara baada ya kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya ASEC MimosaS na kwenda sare ugenini nchini Niger dhii ya USGN.

Aidha mkongwe huyo pia aliendelea kusema kuwa, katika maandalizi yao chini ya kocha wao Mkuu Pablo, walipa muda wa kutazama baadhi ya michezo ya wapinzani wao kabla ya kuwakabili siku ya kesho.

“Tumeangalia mechi zao mbili walizocheza, ni timu moja nzuri na sisi tumejiandaa kwa hilo na sisi tuatapamabana, kila mtu yupo tayari na tumejiandaa kwa mchezo, wapo watarajia mazuri kutoka kwenye timu yao”. Alisema Nyoni

Kwa upande wa kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa Ghana Benard Morrison yeye kwa upande wake alifunguka kuwa Simba ni timu kubwa kwa sasa na wapo tayari kwa mchezo huo.

“Simba ni timu kubwa bna kila mtu hapa ni mchezaji kubwa na tupo tayari kwa mchezo” alisema Morrison

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!