Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yashikwa shati na JKT, Lamine Moro kuikosa Azam FC
Michezo

Yanga yashikwa shati na JKT, Lamine Moro kuikosa Azam FC

Spread the love

TIMU ya Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa mzunguko wa pili Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mchezo huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe na Katibu wa wizara hiyo, Dk. Hassan Abbas na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika.

JKT ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 36 ya mchezo,kupitia kwa mlinzi wake wa kulia, Michael Aidan na Yanga kusawazisha katika kipindi cha pili kupitia kwa winga wao Patrick Sibomana dakika ya 76.

Mchezo huo ulikuwa wa nguvu na kugubikwa na vurugu nyingi kiasi cha beki wa kati wa Yanga, Lamine Moro kutolewa nje baada kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga teke kiungo wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto dakika ya 89.

Katika taflani hiyo Kazimoto nae aliotolewa nje kwa kadi nyekundu mara baada ya kuleta vurugu uwanjani hapo.

Lamine atakosa mchezo ujao dhidi ya Azam FC  utakaopigwa siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha pointi 55 baaada ya kucheza michezo 29 na kusalia kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

error: Content is protected !!