WAJASIRIAMALI nchini wanatakiwa kuwa na bima za biashara ili wanapopatwa na majanga mbalimbali yakiwemo moto,ugonjwa waweze kufidiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yalielezwa Jana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bima ya Fortis, Maryam Shamo alipokua akizungumza na waandishi wa habar wakati wa uzinduzi wa Malkia Bima uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Fortis kwa kushirikiana na Assemblies Bima Jana walizindua huduma ya Malkia akaunti kwa lengo la kujinufaisha mjasiriamali mwanamke kufikia malengo yake akiwa na ulinzi wa Bima hiyo.
Maryam alisema kuwa Fortis kwa kushirikiana Assemble imeamua kufanya hivi kwa lengo la kuwanufaisha wanawake mmoja mmoja au kwenye vikundi.
“Wanawake kwenye vikundi kwa kama vile vikoba,saccos ,vikundi vya akina mama na wafanyabiashara wanapopata maafa yanayosababishwa na moto na viashiria vya hatari zake,kukatizwa kwa biashara kunakotokana na moto au kuvamiwa na majambazi,” alisema Maryam.
Alisema Malkia Bima inafaida kubwa ikiwa ni pamoja na ushauri wa afya baada ya maafa ya moto,gari wagonjwa pindi ajali ya moto inapotokea ,ajali binafsi,kulipiwa fedha hospital pindi mtu anapopatwa na maradhi na huduma nyinginezo.
Ameeleza kuwa Malkia.linda akaunti ni rahisi kufungua na inagharimu kiasi cha shilingi 8000 tu.
Naye Tabia Massudi Mkurugenzi wa Bima ya Inssuarance alisema wameamua kuungana pamoja ili kuunga mkono jitihada za serikali kwamba kila mtanzania awe na Bma.
Hata hivyo alisema licha ya kwamba boma anajulikana kama Malkia lakini kila mjasiriamali anufaike nayo mwanamke na mwanaume
Leave a comment