Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri mkuu kufanya ziara ya siku 3 mkoani Songwe
Habari za Siasa

Waziri mkuu kufanya ziara ya siku 3 mkoani Songwe

RC Songwe
Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Songwe kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi pamoja na watumishi wa umma. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 21 Novemba 2023, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk. Francis Michael amesema kuwa, Waziri Mkuu atawasili mkoani Songwe kesho tarehe 22 Novemba 2023 na atahitimisha ziara yake tarehe 25 Novemba 2023 ambapo atetembelea Wilaya mbili za Ileje na Mbozi.

Dk. Francis alibainisha tarehe 23 Novemba 2023 Waziri Mkuu atakagua miradi miwili, kuweka mawe ya msingi ya miradi miwili pamoja na kuzungumza na wananchi wilayani Ileje.

Dk. Francis aliongeza kuwa tarehe 24 Novemba 2023,  Waziri Mkuu atakuwa wilayani Mbozi ambapo atazindua mradi mmoja, kukagua miradi miwili, kuweka jiwe la msingi mradi mmoja pamoja na kuzungumza na wananchi.

Alibainisha kuwa siku ya tarehe 25 Novemba 2023 Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara yake, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na watumishi wote wa Mkoa wa Songwe ambapo majumuisho hayo yatafanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Dk. Francis ameeleza kuwa ziara hiyo ya Waziri Mkuu mkoani humo ni muendelezo wa ziara aliyoifanya tarehe 13 hadi 16 Aprili, 2023 ambapo alitembelea Halmashauri tatu za Momba, Songwe na Tunduma na sasa anakuja kumalizia halmashauri ya Ileje na Mbozi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!