Thursday , 13 June 2024
Home Habari Mchanganyiko DC Songwe aitia kufuli kampuni ya utafiti wa madini
Habari Mchanganyiko

DC Songwe aitia kufuli kampuni ya utafiti wa madini

Spread the love

Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Solomon Itunda amesimamisha shughuli za utafiti wa madini ya dhahabu zinazofanywa na Kampuni ya Gold Valley Company Limited katika mto Zira kijiji cha Ileya kata ya Ifwenkenya, wilayani Songwe kutokana na kampuni hiyo kukiuka taratibu na sheria. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Itunda ametangaza uamuzi hu oleo Jumanne baada ya kufanya ziara katika eneo hilo akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya kupokea ripoti ya timu ya wataalam  aliyoiunda kutokana na malalamiko ya wananchi juu ya uchafuzi wa maji ya mto Zira ambayo huyatumia.

Alisema kampuni hiyo pia haikuwa na vibali kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC na Mamlaka ya Bonde la Ziwa Rukwa huku baadhi ya wananchi kulalamika wakidai kuwa maji wanayotumia yamekuwa na kemikali zinazotokana na shughuli hizo.

“Niliunda kamati ya wataalamu kwa niaba ya Kamati ya Usalama ya Wilaya na wakawasilisha ripoti, baada ya  kupitia ripoti ile ilibainisha wazi kwamba kampuni ilianzisha shughuli bila kufuata taratibu za kisheria.

“Kwa kuzingatia ripoti ya timu ya wataalamu tumekuja na maamuzi yafuatayo, kwanza kuanzia leo shughuli zote zinazoendelea kufanyika katika mto huu wa Zira zisimame” alieleza DC Itunda.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) waanze kufuatilia kuanzia walipoanza kufanya utafiti wao na wawasilishe ripoti ofisini kwake.

Kabla ya uamuzi huo, kampuni hiyo ilipewa nafasi ya kurekebisha mapungufu hayo baada ya kamati hiyo kutembelea eneo hilo tareehe 3 Oktoba mwaka huu, lakini hadi kufikia tarehe 16 Novemba 2023 ilikuwa haijatekeleza maagizo hayo.

Itunda ameeleza kuwa Serikali inawapenda wawekezaji lakini wanaofuata taratibu hivyo ameuagiza uongozi wa kampuni hiyo kukamilisha maagizo ili iweze kuendelea na shughuli zake.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Amani Msumba amesema kuwa wamepokea maagizo hayo huku akiahidi kuwa watayafanyia kazi.

“Nashukuru sana kwa ujio wa mkuu wa wilaya na maagizo aliyotuachia. Kwa niaba ya kampuni tutatekeleza yote aliyotuagiza na tutafuata taratibu na zitakapokuwa zimekamilika tutawasiliana naye ili kuendelea na shughuli kama kawaida” alieleza mwakilishi huyo.

Diwani wa Kata ya Infwenkenya, Pius Omboka alisema  pamoja na kampuni hiyo kutokamilisha taratibu lakini ilikubaliana na wananchi wa eneo hilo kabla ya kuanza shughuli hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

GGML yaahidi kuendelea kushirikiana na UDSM kudhamini tafiti, ubunifu

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeahidi kuendelea kushirikiana...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Marekani yasaka fursa uwekezaji sekta ya nishati Tanzania

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amekutana...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chalamila: Wasanii wanamchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa...

error: Content is protected !!