Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mchengerewa asimamisha wakurugenzi Kibaha, Ifakara
Habari za SiasaTangulizi

Mchengerewa asimamisha wakurugenzi Kibaha, Ifakara

Mohamed Mchengerwa
Spread the love

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewasimamisha kazi wakurugenzii wawili wa halmashauri kuanzia tarehe 20 Novemba 2023 ili kupisha uchunguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Wakurugenzi hao ni Butamo Nuru Ndalahwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro Lena Martin Nkaya.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah imesema Mchengerwa amechukua hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya awali ya timu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wakurugenzi hao kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo katika halmashauri zao kwa nyakati tofauti.

Timu hiyo iliyoundwa na Katibu Mkuu kwa maelekezo ya Waziri Mchengerwa imebaini mapungufu ikiwemo kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo.

Butamo Nuru Ndalahwa

Mchengerwa amewasimamisha kazi kwa kuzingatia Kanuni ya 37 (1) na 38 (1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022 ili kupisha uchunguzi wa kina.

Aidha, amewasisitiza Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwa ni pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo.

Mchengerwa ameendelea kusisitiza kuwa hatosita kuchukua hatua stahiki kwa atakayethibitika kutenda kinyume.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!