February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Kairuki akumbuka vyeti feki

Angela Kairuki, Waziri wa Madini

Spread the love

ALIYEKUWA  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki leo ameaga  ofisi yake ya zamani huku akikumbuka alivyohangaika na watumishi waliokuwa na vyeti feki. anaandika Angel Willium.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kairuki amesema katika kipindi cha miezi 23 tangu ateuliwa kuongoza wizara hiyo, amekumbana na changomoto nyingi.

Amesema suala la vyeti feki ambalo liliwakumba watumishi wa serikali wapatao 12,000 ulikuwa ni mtihani mkubwa kwake wakati akiongoza wizara hiyo ambayo ipo chini ya Rais.

“Baadhi ya maofisa utumishi hawakuwa waaminifu walikuwa wanawaficha wale wenye feki,  lakini suala hilo tulilikamilisha kwa kiasi kikubwa,’’ amesema

Kwa upande wake, Waziri mpya wa wizara hiyo, George  Mkuchika ameahidi kuendeleza kasi na nidhamu kwa watumishi wa umma.

Kairuki ameteuliwa kuwa Waziri wa Madini kumrithi mtangulizi wake, George Simbachawene ambaye alitimuliwa kazi kutokana na kutajwa katika ripoti ya Bunge iliyochunguza madini ya Almasi.

error: Content is protected !!