March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Edwin achomoka na milioni 60 tatu mzuka

Mshindi wa mchezo wa bahati nasibu ya Tatu, Mzuka Edwin Kawito wa Dodoma

Spread the love

EDWIN Kawito(25), mkazi wa Manispaa ya Dodoma amekabidhiwa Sh. milioni 60 alizojishindia katika droo ya 10 ya mchezo wa bahati nasibu ya tatu mzuka, anaandika Dany Tibason.

Zawadi hiyo ilikabidhiwa kwa Kawito na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme. Kawito aliibuka mshindi wa mchezo wa bahati nasibu ya tatu mzuka katika droo ya 10.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Kawito, amesema hatazitumia fedha hizo kwa sasa mpaka kwanza apate ushauri wa wataalam jinsi ya kuzitumia fedha hizo.

Amesema amekuwa akicheza mchezo huo mara kwa mara tangu ulipoanza hapa nchini. Ameongeza kuwa amekuwa akicheza mara moja hadi mbili katika juma huku akieleza kwamba katika kipindi cha nyuma aliwahi kufanikiwa kushinda hadi Sh. 300,000.

“Nilikuwa nikicheza na rafiki zangu lakini kuna kipindi nilitaka kukata tama, rafiki zangu walinihamasisha niendelea kucheza wakieleza kuwa nimewahi kushinda nyuma katika droo za saa ukilinganishwa wao,”amesema

Kwa upande wake, Mndeme alimpongeza mshindi huyo na kuishukuru tatu mzuka kwa kufika mkoani Dodoma huku akiwataka Watanzania kucheza mchezo huo.

“Ninayo furaha kuona mshindi wa tatu mzuka kwa kipindi hiki anatokea Dodoma, tunayo imani kubwa kuwa mshindi atabadilisha maisha yake na ya familia yake pamoja na jamii inayomzunguka,” amesema.

Tatu mzuka imefanikiwa kutoa zaidi zinazofikia shilingili bilioni mbili tangu ilipoanzishwa Agosti mwaka huu.

error: Content is protected !!