Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Biashara Wataalam Uganda wapewa darasa teknolojia mpya uchimbaji madini katika maonesho Geita
Biashara

Wataalam Uganda wapewa darasa teknolojia mpya uchimbaji madini katika maonesho Geita

Spread the love

MAONESHO ya Teknolojia ya Madini yamezidi kuwa darasa kwa wadau mbalimbali baada ya wageni kutoka Wizara ya Madini ya Serikali ya Uganda kushiriki na kujifunza namna Kampuni ya GGML inavyotumia teknolojia za kisasa katika shughuli za uchimbaji wa chini kwa chini ya ardhi pamoja na wa wazi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Wageni hao walioongozwa na Mkaguzi wa Migodi katika Kurugenzi ya Utafiti wa Jiolojia na Migodi anayesimamia shughuli za uchimbaji Mashariki mwa Uganda, Morris Muheirwe Tabaaro, walitembelea banda la GGML lililopo katika maonesho hayo ya sita yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili-EPZ mjini Geita.

Akizungumzia dhumuni la kutembelea maonesho hayo, Tabaaro alisema mbali na kubadilishana uzoefu, pia wamekuja kujifunza namna kampuni hiyo inafanya utafiti wa madini, uchimbaji wa madini hiyo kwa njia za wazi na chini ya ardhi.

Mhandisi Mwandamizi wa mipango kazi mirefu na wa chini ya ardhi kutoka GGML, Emanuel Njabugeni (kushoto) akiwaelezea wageni kutoka nchini Uganda namna GGML inavyotumia teknolojia mbalimbali katika uchimbaji wa wazi na wa chini kwa chini ya ardhi.

Aidha, akizungumzia darasa alililowapatia wageni hao kutoka Uganda, Mhandisi Uchimbaji Mwandamizi wa mipango kazi mirefu na wa chini ya ardhi kutoka GGML, Emanuel Njabugeni alisema hatua hiyo imedhihirisha kuwa Tanzania imezidi kuwa mfano wa kuigwa katika shughuli za uchimbaji kupitia miongozo mbalimbali iliyowekwa na hata kufikia dira ya Taifa.

Njabugeni mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika shughuli hizo za uchimbaji, alisema katika maonesho hayo, wameelekeza wageni, wachimbaji wadogo na washiriki kuhusu matumizi sahihi ya teknoliojia ambazo zinapunguza gharama za uchimbaji lakini pia kulinda mazingira.

“Tuna teknolojia ambazo zimepiga hatua ikiwamo software ya Studio UG for under ground Pamoja na teknolojia nyingine ambazo tumewaelekeza wenzetu wa Uganda namna zinavyoweza kuwapatia faida.

“Wenzetu wa Uganda wanayo haja kubwa kujifunza kutoka kwetu sisi watanzania hasa GGML ambayo ndio mgodi mkubwa Afrika Mashariki kwani unaongoza kiteknolojia na hata uhifadhi wa mazingira.

“Kwa hiyo nimewaelekeza ni kwa namna gani GGML inatumia teknolojia hizi katika kuchimba madini na kuhifadhi mazingira jambo ambalo limekuwa faida kwetu na hata jamii inayotuzunguka kwa ujumla,” alisema na kuongeza;

“Niliwaelezea kuwa kuna kampuni ambazo tunazitumia kwa ajili ya utafiti hapa Geita, mfano GGML tunatumia kampuni ya Capital Mining Services ambao wakishatupatia hizo data tunajua kwamba hapa tutachimbaji kwa faida au hasara. Kwa kuzingatia bei ya dhahabu, vifaa ambavyo tutavitumia na gharama za rasilimali watu na gharama mbalimbali kama kujaza mashimo na kuacha mwamba katika mazingira salama.”

Hatua hiyo inakuja wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kutekeleza dira ya 2030 ambayo imeanzishwa na Waziri wa Madini, Athony Mavunde ambaye amelenga kuhakikisha madini yawe ni utajiri na maisha ya watanzania

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Shinda mtonyo mrefu ukicheza Shaolin Crew kasino ya  Meridianbet

Spread the love  TAIFA la Uchina limebebwa na historia kubwa sana, wengi...

Biashara

Kasino ya Lucky Sevens ni rahisi kucheza na kuibuka tajiri, fanya haya

Spread the love  NENO Kasino unapolisikia kwa mara ya kwanza unapata picha...

Biashara

Ujenzi waiva barabara ya Bigwa – Kisaki

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa mkandarasi atakayetekeleza ujenzi...

Biashara

Fanya haya kabla hujacheza kasino

Spread the love  UNAPOANZA kufikiria jinsi ya kutengeneza pesa kirahisi usipate shida,...

error: Content is protected !!