Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wanne Chadema wachuana ubunge Kinondoni
Habari za Siasa

Wanne Chadema wachuana ubunge Kinondoni

Spread the love

WANACHAMA wanne wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamejitosa katika kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge Kinondoni jijini Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Watia nia hao, leo Jumatatu tarehe 13 Julai 2020, wanapigiwa kura za maoni na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo hilo ambalo kwa sasa mbunge anayemaliza muda wake ni Maulid Mtulia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wanaochuana kwenye mbio hizo ni; Susan Lyimo, Mbunge Viti Maalum, Moza Ally, Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Mbesi Mombeki na Rose Mushi, Diwani wa Viti Maalum.

Mchakato huo wa kura za maoni unaoendelea katika Ukumbi wa Garden, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, unasimamiwa na Kubra Abdallah.

Kura za maoni ndani ya Chadema kwa ajili ya kupata wagombea ubunge, zimeanza baada ya shughuli ya uchukuaji na urudishaji fomu  kufungwa tarehe 10 Julai 2020.

Kwa sasa wajumbe wanaendelea kupiga kura.

Baada ya shughuli ya kura za maoni kufungwa, Kamati Kuu ya Chadema itaketi tarehe 30 hadi 31 Julai 2020, kwa ajili ya kuteua wagombea ubunge wa chama hicho, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Kwa mujibu ya ratiba iliyotolewa na Chadema, kura za maoni kwa wabunge zimeanza leo hadi tarehe 17 Julai 202

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!