October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanawake watakiwa kupuuza misemo ya kukatisha tamaa

Spread the love

MISEMO ya kuvunja moyo wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye siasa imetakiwa kupuuzwa na wanawake wenyewe huku ikiwa ni njia ya mapendo kwao kwenye kuleta manufaa kisiasa. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mwezeshaji wa masuala ya uongozi na jinsia kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP- Mtandao, Dk. Consolata Sulley alisema misemo kama adui wa mwanamke ni mwanamke haina budi kupuuzwa kwani hakuna ukweli wowote wa uadui baina ya mwanamke na mwanamke bali waendelee kushikana.

Dk. Sulley ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema wanawawake hawana budi kuacha kuogopa misemo ya kuvunjika moyo inayotolewa na watu kwani mambo ya kuvunjana moyo yapo hata kwenye familia mbalimbali kwa lengo au malengo na faida ya watu wachache.

Alisema mada juu ya jinsia inaeleza tofauti za kimajukumu katika mwanaume na mwanamke na wakati mwingi katika jamii wigo wa kisiasa unaaminika kuwa ni wa mwanaume pekee na kumbe si kweli na ukweli ni kwamba wigo huo ni wa wote.

Dk. Sulley alisema, zipo aina nyingi za kuvunjwa moyo sio tu kwa msemo huo bali pia hata kwa kukatishwa tamaa kwa kunyanyaswa, kudhalilishwa, kutolewa habari au taarifa za kuvunja moyo kwenye vyombo vya habari.

Dk. Sulley anasema pia kuna kukatisha tamaa kwingine kwa njia ya vurugu, hivyo anawaasa wanawake kutovunjika moyo na kutorudi nyuma na kuhakikisha kuwa wanatimiza malengo yao.

“Msemo wa Adui wa Mwanamke ni mwanamke usiwagawe wanawake kwenye nafasi za uongozi sababu hauna nguvu yoyote kwa wanawake bali ni msemo wa kisiasa,” anasema.

Anasema, msemo huo ni dhana ya watu ili kuwatenganisha wanawake na kufanya nguvu yao kuwa chini na kukosa nafasi za chaguzi kufuatia uwingi wa wanawake nchini kutolingana na wanaume ambao wanaogopa kushindwa na kibua misemo ya kuvunja moyo.

Dk. Sulley alisema haaamini dhana hiyo kabisa kutokana na kutengenezwa na kuwataka wanawake kutouingiza huo usemi katika msamiati wa lugha bali wajitazame wao kama watu wanaoweza kusirikiana na kufikia malengo yao. 

error: Content is protected !!