Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wananchi Manyara wamuahidi ushindi Rais Samia 2025
Habari za Siasa

Wananchi Manyara wamuahidi ushindi Rais Samia 2025

Spread the love

WANANCHI wa Mkoa wa Manyara, wameahidi kumchagua kwa kishindo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika uchaguzi mkuu wa 2025, kutokana na kazi kubwa aliyofanya kuwapelekea miradi ya maendeleo iliyoboresha upatikanaji wa huduma za kijamii hususan maji na afya.Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara…(endelea).

Ahadi hiyo imetolewa na wananchi wa Manyara, wakizungumzia ujio wa Rais Samia mkoani humo, ambaye anatarajia kufanya ziara ya kikazi tarehe 14 Oktoba 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Queen Sendiga, amesema Serikali ya Rais Samia  imepeleka Sh. 535 bilioni ndani ya muda mfupi, kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maendeleo hususan ya maji, ambapo kuna miradi miwili inayogharimu Sh. 62 bilioni, inatekelezwa.

“Tunajua tarehe 14 Oktoba itakuwa siku ya kipekee kwa wananchi wa Manyara kama ingewezekana kukutana uso kwa uso na Rais Samia, wangemwambia tunakushukuru kwa miradi mikubwa ya maendeleo aliyoleta katika mkoa wetu. Wananchi hawana cha kukulipa tunasubiri 2025 twende tukakulipe kwa kazi kubwa uliyofanya,” amesema Sendiga.

Sendiga amesema mabilioni ya fedha yaliyopelekwa Manyara na Serikali ya Rais Samia, yanatumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali, ikiwemo ya afya na elimu.

“Tuna shule kubwa za kisasa na nzuri zimejengwa kwa kipindi hiki kifupi. Miradi ya hospitali, vituo vya afya na maji inasaidia Manyara, sababu wananchi wake ambao ni wafugaji kwa muda mrefu wamepata tabu ya maji, lakini sasa wanapata maji na majosho ya wanyama wao yamejengwa,” amesema Sendiga.

Kwa upande wake Felista Thomas amesema “namshukuru sana Rais Samia katupatia mradi wa maji kijiji kwetu kwani kwa muda mrefu tulikuwa tunateseka maji hakuna. Hatuna cha kumlipa zaidi ya 2025.

Dativa Damia, ambaye anasema ameamua kumuita mtoto wake wa kike jina la Samia kutokana na kuridhishwa na uchapakazi wake, amesema tangu ameingia madarakani Serikali yake imeleta maendeleo mkoani humo.

“Nimeamua kumuita mwanangu Samia kutokana na maendeleo niliyopata mimi binafsi tangu Rais Samia ameingia madarakani lakini pia maendeleo ninayoana kwa Mkoa wa Manyara kwa ujumla,” amesema Dativa.

Mfanyabiashara mkoani humo, Alex Olomi, amesema tangu Rais Samia aingie madarakani amefungua fursa za kiuchumi na kuwezesha vijana kujiajiri.

“Tangu umeingia madarakani tumepata fursa ya kimaendeleo, vijana wengi  tumepata fursa nyingi za kibiashara na kilimo. Ukatuletea ghala la chakula mazao yetu yaliyoko mashambani tunauza mjini, umetujengea barabara za mitaa zimekaa vizuri, kila nyumba zina umeme na hospitali zina kila kitu,” amesema Olomi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!