Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi KIA walia kunyang’anywa ardhi
Habari MchanganyikoKitaifa

Wananchi KIA walia kunyang’anywa ardhi

Spread the love

WANANCHI wa vijiji vinavyozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, (KIA), wamelalamikia serikali kwa kudai kuwanyang’anya ardhi bila kuzingatia sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea.)

Aidha, wananchi hao wanapinga kuitwa wavamizi kwenye eneo hilo kwa kile walichodai kuwa mwaka 1969 aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati, Julius Nyerere alifika hapo na kufanya kikao na wazee wao ambapo walikubali kumpa ardhi hekta 460 ambazo mpaka sasa hawajaziendeleza zote hivyo si sawa kuwaita wavamizi.

Wananchi hao wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakifanya mahojiano na wandishi wa habari waliowatembelea kwenye makazi yao hivi karibuni ambapo walishuhudia gari la polisi likiwa na polisi wenye silaha na gari la maji ya kuwasha vikiwa vimeegeshwa pembeni ya barabara kwenye kijiji cha Tindigani kata ya Kia.

Mzee Moses Ole Munga mkazi wa Kijiji cha Tindigani alilalamikia, Serikali kuwaondoa kwenye ardhi yao ya asili kwa lazima na haiwaelezi inawapeleka wapi jambo alilodai kuwa wamekuwa kama watoto yatima ndani ya Taifa lao.

“Mimi nina miaka 64 nimezaliwa hapa sijui serikali inatufikiriaje, inatunyang’anya mashamba yote tunayolima, na kulisha watoto.

Wanasema sisi tumevamia Uwanja KIA, wakati uwanja wa ndege umeanza kujengwa sisi tuko hapa ni vijana wadogo tunauona, “ alisema Ole Munga na kuongeza.

…Hatuelewi utaratibu, hawataki hata kutusikiliza inashangaza sana. Mwanzo Mwalimu Nyerere alizungumza na wazee wetu wakampa hekta 460 hawajamaliza kuzitumia sasa wanatunyang’anya hizi nyingine..Hakuna nchi yenye uwanja wa ndege wenye eneo kubwa kama hili”.

“Hapa tumeshaongea na viongozi wengi (Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana wakati akiwa katibu mkuu wa CCM, Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa wanatusikiliza na mara zote wamekuwa wakituambia watatuletea majibu lakini hawajarudi tena,”.

“Mimi sihitaji fedha haiwezi kunisaidia, nahitaji mashamba yangu yananisaidia kutunza familia. Nimezaliwa hapa, nimekulia hapa, nikaoa nikiwa hapa, nikapata watoto na mke wangu mkubwa akafariki nikaoa mwingine naishi naye sasa hivi naye amezeeka. Sijui tunavyoondolewa hapa naenda naye wapi kuaza maisha sijui tutaanza maisha kinamna gani,”.

Mwananchi mwingine wa kijiji cha Chemka kata ya Masama Tundugai, Aziza Juma alisema amezaliwa kabla ya uwanja wa KIA haujajengwa, hivyo anashangaa kusikia akiwambiwa aondoke aneo hilo kwa madai kuwa ni wavamizi.

“Wamekuja wameandika namba kwenye mlango wakatuhesabu pamoja na watoto wangu wakahesabu miti, migomba na makaburi wamekuta hapa makaburi karibu 40 wanasema ardhi ni ya serikali hivyo hawawezi kutupa fidia ya ardhi.
Wakati KIA imeanza kujengwa mimi nilikuwa naiona nilikuwa na umri mdogo. Nilikuwa nachuma mchicha naenda kuuza kule wakajenga wakamaliza wakapanda ile mijohoro wakasema mwisho wa KIA utakuwa hapo baadaye wakasema mwisho wa KIA utakuwa barabara ya Naiberera sasa wanasema inakuja mpaka huku Chemka,” alisema, Esther Thomas (67), mwanakijiji wa Chemka.

…Sasa KIA iko mbali zaidi ya kilometa 15 kutoka hapa eneo hilo lote mpaka uje uingie huku mashambani unajiuliza watakuja kuegesha ndege?. Sisi tumeshangaa hapa juzi tumevamiwa na askari karibu 40 na magari zaidi ya nane hatukupewa nafasi ya kusikilizwa unaambiwa sema hivi mimi sikuweza nilishikwa na presha nikashindwa,”

“Serikali ituambie kwa nini tunavamiwa kwenye kijiji chetu cha Chemka hatuko kata ya KIA tuko kata ya Rundugai. Sasa tunashangaa wanaunganisha na kata ya Kia. Mimi na familia yangu tunamiliki ekari 40 ambazo tunazitumia kwa makazi na kilimo,”.

Akizungumzia sakata hilo Wakili, Denis Moses alisema sheria ya ardhi sura ya 113 na ya ardhi ya vijiji na sheria ya utwaaji wa ardhi sura ya 118 zote zinatoa muongozo huku sikisisitiza kuwa kila mtu anahaki ya kukalia ardhi bila kubughudhiwa na mtu yeyote.

“Ikitokea kuna haja kwa lengo mahsusi sana ardhi inatakiwa kuchukuliwa kuna taratibu za kufuatwa. Sheria imeweka bayana kuwa itabidi kuwe na mazungumzo, ili watu walipwe fidia kwa kupewa ardhi mbadala lakini imesisitiza utawaondoa watu ikiwa kuna jambo mahsusi linalokulazimu kuichukua ardhi hiyo,” alisema Wakili Moses na kuongeza.

… Inatakiwa afike mthamini kuithaminisha ardhi hiyo, lazima wananchi wanaoishi kwenye hiyo ardhi washirikishwe wanaporidhia ndipo mchakato huo unaweza kuendeleza,” alisema.

Akijibu hoja hizo za wananchi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu alisema kuwa uwanja huo ni mali ya serikali na una hati ya miaka 99 ambapo kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu kuna wananchi waliingia kwenye eneo hilo kwa kujua au kutojua.

Alisema wameamua kuweka mipaka kwa mujibu wa sheria kulingana na hati iliyopo na wameshamaliza zoezi hilo kwa upande wa Kilimanjaro na Arusha ambapo kwa sasa zoezi linaloendelea ni la tathmini.

Babu alisema kuwa wananchi hao walishirikishwa na wakati akiapishwa kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro, mbunge wa jimbo la Hai, Saashisha Mafue alikuwa akifanya kikao na wananchi hao aliwaeleza suala la uwekaji mipaka, hivyo amefanya vikao sita na wananchi, viongozi wa kijiji na viongozi wa mila Malaigwanan.

…Kwamba wanafanyiwa tathmini ya nyumba, migomba na makaburi ni sawa kwa sababu ardhi ile ni ya serikali na ina hati ya miaka 99. Kinachofanyika ni huruma ya Rais kwa wananchi wake kuwa wale waliovamia basi tuwape chochote wasiende kuhangaika,”.

RC Babu alisema kuwa mambo mengine yanaweza kuja endapo viongozi wa juu wataangalia kuwa walikuwa watu hao walikuwa hapo muda mrefu walikuwa wanalima lakini kwa sasa utaratibu ndiyo huo huku akiwataka wananchi watoe ushirikiano.

“Baada ya kuzindua bikoni ya kwanza mimi nimeenda Rombo kukagua ujenzi wa madarasa huku nyuma wamevunja magari ya serikali vioo, wamempiga DC, wamempiga mwenyekiti wao wa kijiji na watu wengine,” alisema RC Babu.

…Wanataka kuichezea serikali sisi watupige tuwaache tu? yaani wananchi mtupige viongozi wa serikali sisi tuwatizame tu? kwa hiyo ndiyo maana mimi nimeongeza askari,”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

error: Content is protected !!