Thursday , 7 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wanafunzi waliofanya mtihani wakiwa na watoto wachanga wamkuna Jokate
ElimuHabari za Siasa

Wanafunzi waliofanya mtihani wakiwa na watoto wachanga wamkuna Jokate

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzani (UWT), Jokate Mwegelo amesema hatua ya wanafunzi walioruhusiwa kufanya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2023 huku wakiwa na watoto wachanga, ni uamuzi wa kipekee ambao umefufua ndoto za mabinti hao. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema uamuzi huo ambao uliasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, umelenga katika kuhakikisha kila mwanafunzi anatimiza ndoto yake kupitia elimu.

Joketi ametoa kauli hiyo leo Jumamosi alipotembelea eneo la Chamazi Magengeni Jijini Dar es salaam na kukutana na binti aliyefanya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2023 huku akiwa ananyonyesha.

Mbali na binti huyo, pia Jokate amekutana na binti mwingine anayeishi maeneo ya Mbande Jijini Dar es salaam ambaye na yeye amefanya mitihani huku akiwa ananyonyesha mtoto mwenye siku nane.

Aidha, mbali na kuwapongeza kwa jitihada za kufanya mtihani huo, Joketi pia ametoa wito kwa wazazi kuzingatia malezi bora ya watoto ili kuwaepusha na mimba za utotoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!