Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wanafunzi 14 kidato cha pili wafutiwa matokeo kwa kuandika matusi
ElimuHabari

Wanafunzi 14 kidato cha pili wafutiwa matokeo kwa kuandika matusi

Spread the love

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limefuta matokeo yote ya wanafunzi 14 walioandika matusi katika mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa kidato cha pili wa mwaka 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Mtendaji Mkuu wa NECTA, Athuman Amasi, wakati akitangaza matokeo ya mitihani hiyo iliyofanyika Oktoba na Novemba 2022.

Aidha amesema baraza limefuta matokeo yote ya wanafunzi 52 wa kidato cha pili baada ya kubainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo.

Katika hatua nyingine baraza limefuta matokeo yote ya wanafunzi 213 wa darasa la nne baada ya kubainika kufanya udanganyifu.

“Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5(2)

9(i) na (j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani suura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2) (b) cha kanuni za mitihani za mwak 2016,” amesema Amasi.

Ameongeza kuwa Baraza limevifunia vituo viwili vya mitihani vilivyothibitika kupanga na kufanya udanganyifu katika Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la nne .

Ametaja vituo hivyo vilivyopo Mwanza kuwa ni Busara S/M kilichopo Halmashauri ya Magu na Musabe S/M kilichopo Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Amesema vituo hivyo vimefungiwa kwa mujibu wa kifungu cha 4(8) cha Kanuni za Mitihani mwaka 2016 hadi hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa Mitihani ya Kitaifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

error: Content is protected !!