Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Baraza la ardhi Kinondoni laipiga ‘stop’ Manispaa kujenga eneo lenye mgogoro
Habari Mchanganyiko

Baraza la ardhi Kinondoni laipiga ‘stop’ Manispaa kujenga eneo lenye mgogoro

Spread the love

BARAZA la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni limetoa amri ya zuio ya ujenzi wa Kituo cha Afya eneo la Tegeta ‘A’ Goba jijini Dar es Salaam. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Amri hiyo imetolewa tarehe wiki iliyopita na Mwenyekiti wa Baraza hilo Longinus Rugarabamu baada ya waombaji kuwasilisha zuio hilo kupitia wakili wao Dickson Matata.

Maombi ya msingi kwenye shauri hilo ni kulitaka baraza litamke mmiliki halali wa eneo hilo na limkabidhi haki ya kisheria ya umiliki pamoja na kinga ya Mahakama  sambamba na maombi madogo ya kuzuia ujenzi wa kituo cha afya unaondelea kwenye kituo hicho.

Waombaji wanadai kuwa uongozi wa Kata pamoja na Manispaa ya Kinondoni umechukua eneo hilo kimabavu bila kufuata sheria na kutoa haki kwa wamiliki.

Waombaji kwenye shauri hilo ni pamoja na Romanie Mosha, Godfrey Roman, Rumishael Roman na George Mazewa na wadaiwa wakiwa ni Mtendaji wa Kata ya Goba, Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni, Tabia Mziwanda na Mrisho Ramadhani.

Akitoa amri hiyo Mwenyekiti Rugarabamu alisema “Ombi la zuio hilo limekubaliwa wajibu maombi, watumishi au mawakala wao hawaturuhusiwa kufanya shughuli ya uendelazaji eneo hilo mpaka shauri la msingi litakaposikilizwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!