Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wamesahau aliyofanya Magufuli
Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Wamesahau aliyofanya Magufuli

Hayati Rais John Magufuli
Spread the love

JUMATATU ya tarehe 16 Oktoba 2023 itabaki kuwa siku ya kumbukumbu kwa wananchi wa kizazi hiki wakazi wa mkoa wa Singida. Hiyo ndiyo siku walifanya maadhimisho ya miaka 60 ya kuzaliwa/ kutangazwa mkoa huo tarehe 16 Oktoba 1963. Anaandika Joster Mwangulumbi…(endelea).

Kilichoonekana sherehe zililenga kumnadi Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya uchaguzi ujao. Walimsifu kwa namna alivyotoa (mfukoni) mabilioni ya shilingi za walipakodi wa Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa barabara, shule, zahanati, na usambazaji maji.

Kusema kweli, hakuna binadamu ambaye hapendi kusifiwa, pia hakuna binadamu ambaye anataka kusikia ukosoaji. Kwa hiyo, walichokifanya Singida kumsifu, na hata kufikia kumwomba akubali kuitwa “Mama wa Taifa” ni ubinadamu uleule.

Askofu Cyprian Hilinti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kati Singida aliyewasilisha ombi kutaka Samia aitwe Mama wa Taifa alitoa hoja. Kama wapo wanaopinga, nao watoe hoja ili yeye aamue. Lakini mbona hata sasa anaitwa mama! Aliombwa na nani? Au askofu alitaka kuonesha na yeye ni chawa wa mama?

Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli

Jukumu la Mwalimu Nyerere lilikuwa kututoa kwenye makucha ya ukoloni na kutuweka pamoja kama Taifa. Alifanikiwa kuyaunganisha makabila yote 120 kuwa taifa na kufanya kampeni kubwa kuondoa udini, ukabila na tofauti za kipato. Hivyo, haikuwa ajabu Watanzania kumwita Baba wa Taifa. Wengine watapewa heshima hiyo kwa lipi?

Jukumu la marais waliomrithi lilikuwa kuleta maendeleo: Kujenga nchi kiuchumi; kutuondoa katika lindi la umasikini, kupambana na maradhi na ujinga.

Kwa viwango tofauti marais Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli walijenga barabara, madaraja, walisambaza maji, waliboresha kilimo, ufugaji na uvuvi. Mfano Mkapa alianzisha TRA, Takuru (baadaye Kikwete akaboresha ikaitwa Takukuru), na Ofisi ya CAG.

Ukusanyaji mapato uliongezeka kuanzia awamu ya Mkapa. Kikwete alizunguka dunia nzima kutafuta wawakezaji. Baadhi yao, akiwemo Dangote, waliitikia haraka wakajenga viwanda vyao, wakaanza kulipa kodi. Pato la Taifa liliongezeka na bajeti ikaongezeka.

Bajeti ya Magufuli ilikuwa kubwa na bajeti ya mama Samia ni kubwa zaidi sasa anaweza hata kufanya sherehe za miaka 60 ya mkoa wa Singida huku tukisubiri sherehe kama hizo katika mikoa mingine 26.

Kitabu cha mapato cha Samia kinasomeka vizuri – anatoa mabilioni ya shilingi kwa ajili ya barabara, maji, shule na zahanati – kwa sababu watangulizi wake Magufuli na Kikwete walitengeneza msingi wa kuongeza mapato.

Fedha za sherehe zipo, lakini za kuondoa umaskini Singida hazipo. Singida ni moja na mikoa masikini lakini inafanya sherehe nzito. Singida bado ina njaa lakini inafurahia. Kasi ya maendeleo ni ndogo Singida, lakini inafanya sherehe.

Singida wanadai hawana shida, lakini Samia akawaambia hakuna siku matatizo yatakwisha kwa kuwa watu wanaongezeka. Singida wanadai wameridhika, lakini Samia anawaambia kwa namna Singida ilivyo, kasi haitoshi.

Sherehe zisizo na maana kama hizi si Magufuli alikuwa anazikataa? Mara hii CCM wamesahau?

2 Comments

  • Takukuru ilikuwepo tangu enzi za Nyerere. Ukiripoti tukio au walioshukiwa kwa rushwa walikuwa wanahojiwa, wanasimamishwa kazi kwa manufaa ya umma. Wengine, walikuwa wanahamishwa kazi.
    Leo, zimekuwa taasisi lakini hazifanyi uchunguzi kama zamani.
    Mbona kuna kesi za miaka 20, 30 na zaidi mahakama ya ardhi! Enzi zile hazikuwepo. Pia watu matajiri hawakuvamia viwanja vya park. Leo hii, Msasani haina park…zimevamiwa na kujengwa majumba!
    Mahakama zimekuwa uchochoro wa matajiri!
    Kama sivyo, kesi za ardhi zimalizwe na matapeli wapigishwe faini.
    Serikali inapoteza fedha nyingi sana humu kwenye kesi kwa sababu shughuli zilizopangwa kuingiza pato la serikali zimesimama….kusubiri kesi za matapeli!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!