Sunday , 3 December 2023
Home Kitengo Biashara Wamachinga Kivule walianzisha
Biashara

Wamachinga Kivule walianzisha

Spread the love

SAKATA la wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) eneo la Kivule kuvunjiwa na vibanda vyao Kisha mali kuchukuliwa na mgambo limechukua sura mpya baada ya kuzifuatilia na kuzikuta Ofisi za Jiji la Ilala zikiwa pungufu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Jana Jumapili, wakizungumza na waandishi wa habari, wamachinga hao wamemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ahakikishe mali zao wanazipata la sivyo watalifikisha sakata hilo kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya wafanyabiashara wamedai kuwa, katika nyakati tofauti walifika ofisini hapo wakiwa na matumaini ya kupata mali zao zote, lakini jambo la kushangaza wamekuta baadhi ya mali hazipo.

Bihimba Mpaya, alidai “tunaishukuru Serikali kwa kuanza kushughulikia suala hilo, lakini tunashangaa kuona kwamba wafanyabiashara wanapata mali pungufu. Tunamtaka Mkuu wa Wilaya atuambie mali ziko wapi, lakini hao waliozichukua wanawajibishwaje.”

Kaimu Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, aliyejitambulishwa kwa jina la Swaleh, alimuomba Rais Samia aingilie Kati ili mali zao zipatikane.

Wafanyabiashara hao wamechukua hatua hiyo baada ya ziara ya Mpogolo, alyefika eneo hilo wiki iliyopita kushuhudia uharibifu huo na kuagiza hatua zaidi kuchukuliwa kwa wahusika, huku akikana kwamba sio maagizo ya Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Shinda mtonyo mrefu ukicheza Shaolin Crew kasino ya  Meridianbet

Spread the love  TAIFA la Uchina limebebwa na historia kubwa sana, wengi...

Biashara

Kasino ya Lucky Sevens ni rahisi kucheza na kuibuka tajiri, fanya haya

Spread the love  NENO Kasino unapolisikia kwa mara ya kwanza unapata picha...

Biashara

Ujenzi waiva barabara ya Bigwa – Kisaki

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa mkandarasi atakayetekeleza ujenzi...

Biashara

Fanya haya kabla hujacheza kasino

Spread the love  UNAPOANZA kufikiria jinsi ya kutengeneza pesa kirahisi usipate shida,...

error: Content is protected !!