Tuesday , 14 May 2024
Home Kitengo Biashara Wajasiriamali Morogoro waomba kuwezeshwa kumudu soko la ushindani
Biashara

Wajasiriamali Morogoro waomba kuwezeshwa kumudu soko la ushindani

Spread the love

Wajasiriamali wanawake mkoani Morogoro wamewaomba wadau wa ukuzaji wa biashara kutoishia mijini badala yake wafike pia vijijini kutoa elimu na usaidizi wa ukuzaji biashara ili kuwajengea uwezo kuzalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika na zinazoweza kukabili ushindani wa soko ya ndani na nje ya nchi. Anaripoti Victor Makinda … (endelea).

Wajasiriamali hao waliyasema hayo jana Jumatatu wakati wakizungumza katika mafunzo ya wajasiriamali wanawake kuhusu kanuni, taratibu na sheria za kufanya biashara kwenye soko la Afrika (AICFTA) yaliyoandaliwa na chemba ya wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC) ulifanyika mjini hapa.

Katibu Tawala Msaidizi upande wa Biashara, viwanda na uwekezaji, Mkoa wa Morogoro, Beatrice Njawa akizungumza kwenye mafunzo ya wajasiriamali wanawake yanayoendeshwa na Chemba ya Biashara Tanzania (TWCC) mjini Morogoro.

Mmoja wa wajasiriamali hao Eva Kipalile mkazi wa Kijiji cha Mbingu kata ya Igima Wilayani Mlimba alisema, licha ya kuzalisha vikapu, ungo na mazao aina ya kakao bado wanakabiliwa na changamoto ya kukosa masoko ya nje kutokana na kukosa nembo ya kuhakiki ubora (TBS), misimbomilia(Barcodes) na usajili wa urasimishaji biashara kutoka BRELA.

Naye Makamu Mwenyekiti wa TWCC Taifa, Rose Romanus alisema ajenda yao ni kuhakikisha wanawake wanapata pesa kwa kutimiza malengo waliyojiwekea kwa kulifikia soko huru la Afrika.

Akifungua mafunzo hayo Katibu tawala Msaidizi upande wa biashara, viwanda na uwekezaji mkoani hapa, Beatrice Njawa aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuzalisha bidhaa zenye ubora zinazokidhi viwango vya masoko likiwemo soko huria la Afrika linalohudumia nchi 54.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Moduli ya kuwasilisha rufaa za zabuni kieletroniki kuanza Julai

Spread the loveMamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imesema moduli...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mshindi ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ akabidhiwa trekta

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imehitimisha msimu wa tatu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hati Fungani ya NMB Jamii yaanza kuuzwa Soko la Hisa London

Spread the loveBenki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya...

Biashara

Vuna mapene hadi Mil 400 ukicheza Expanse Tournament 

Spread the love  Promosheni ya kuvuna mahela ya Meridianbet bado inaendelea kusaka...

error: Content is protected !!