Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wagombea CUF bunge la EALA wachezeana rafu
Habari za SiasaTangulizi

Wagombea CUF bunge la EALA wachezeana rafu

Spread the love

WAGOMBEA Ubunge wa Afrika Mashariki kupitia Chama cha Wananchi CUF wamedaiwa kuchezeana rafu baada ya baadhi yao kujipenyeza kwenye makundi ya wabunge na kupiga kampeni chini kwa chini. Anaripoti Apaikunda Mosha, TUDARco…(endelea).

Itakumbukwa kuwa tarehe 20 na 21 Agosti Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF lilipitisha majina ya wanachama 12 kuwa wagombea wa bunge la Afrika Mashariki na kuagiza Kamati ya Uongozi kuwapanga wagombea hao katika makundi manne kjwa mujibu wa kanuni za uteuzi za chama hicho.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo tarehe 12, Septemba, Katibu Mkuu wa CUF, Hamad Masoud Hamad amesema chama hicho kimepokea taarifa za baadhi ya wagombea kujitangaza wao ni wagombea kupitia kundi moja kati ya hayo manne.

Amesema hayo yanajiri hali ya kuwa Kamati ya Uongozi ya Baraza Kuu la Taifa haijakaa na kukamilisha kazi ya kupanga wagombea katika makundi hayo.

“Chama  kinautaarifu umma kupuuzia taarifa zozote zinazoainisha wagombea wa Ubunge wa Afrika Mashariki kupitia CUF hadi pale chama, kupitia Kamati ya Uongozi wa Taifa kitakapokamilisha kazi yake,” amesema Masoud.

Aidha, imeeleza kuwa ni vema ikafahamika wazi kwamba ni udanganyifu na utovu wa nidhamu kwa mgombea kujipangia kundi na ni kupotosha mamlaka ya vyombo vya kikatiba ndani ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!