Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wakutana kujadili mpango kazi wa uwekezaji miundombinu ya hali ya hewa
Habari Mchanganyiko

Wadau wakutana kujadili mpango kazi wa uwekezaji miundombinu ya hali ya hewa

Spread the love

 

TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Hali ya Hewa ya Denmark (DMI) kama Mshauri na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kama Taasisi ya kusimamia Utekelezaji wa mfuko (Programu) wa kuimarisha miundombinu ya hali ya hewa na ufanisi duniani kwa nchi zinazoendelea (Systematic Observations Financing facility-SOFF) imeandaa warsha ya wadau kujadali mpango kazi wa uwekezaji wa uboreshaji wa miundombinu ya hali ya hewa nchini, tarehe 21 Septemba, 2023, Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), alisema wataalamu kutoka TMA na DMI kwa ushirikiano wa pamoja wameandaa rasimu ya mpango kazi kwa kuzingatia mahitaji ya nchi na kuwakutanisha wadau ili kupata maoni ambayo yatasaidia kuboresha mpango kazi huo.

Aidha, Dk.Chang’a aligusia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa SOFF nchini, mfuko ambao umekuwa ukichangiwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na UNDP.

“Utekelezaji wa mradi huu nchini upo katika awamu tatu ambapo moja ya hatua za awali ni kutambua na kuainisha mahitaji ya nchi katika upande wa miundombinu ya hali ya hewa na kuandaa mpango kazi wa kushughulikia mahitaji yaliyo ainishwa ili koungeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma za hali ya hewa hususani kipindi hiki ambacho tunakabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi,” alisema Dk. Chang’a.

“Hii ni mojawapo ya hatua muhimu ambayo inaenda kuchangia katika jitihada kubwa zinazofanywa na serikali yetu ya kuimarisha huduma za hali ya hewa na kuongeza uwezo wetu wa kuhimili changamoto za mabadiliko hayo ya hali ya hewa. Tunaishukuru sana Serikali na wadau wengine wa maendeleo,” aliongezea Dk. Chang’a.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka DMI, Bw.Christian Rodrup alisema anatarajia kupokea michango muhimu kutoka kwa wadau kwa ajili ya kuboresha rasimu ya mpango kazi, pia alisisitiza kuwa kati ya nguzo nne muhimu za utoaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!