Monday , 13 May 2024
Home Kitengo Biashara Wadau wahimiza kudumisha uwekezaji nishati safi na salama majumbani
Biashara

Wadau wahimiza kudumisha uwekezaji nishati safi na salama majumbani

Spread the love

 

UMOJA wa Wafanyabiashara wa Gesi (LPG) za Mitungi ya Majumbani nchini (TZLPGA) wamekutana na waandishi wa habari kujadili njia endelevu za kukuza sektahio kupitia uwezeshaji wa taarifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Umoja huo ulioanzishwa mwaka 2023 unaundwa na kampuni sita zinazofanya biashara ya gesi za mitungi kwa matumizi yamajumbani ambazo ni CAMGAS, O-GAS, LAKE GAS, TAIFA GAS, ORYX GAS, MANJI GAS na PUMA ENERGY.

Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mjadalahuo, Mkurugenzi Mkuu wa umoja huo, Amos Jackson alinukuliwa, ‘tunaamini kuwa ukusanyaji na usambazaji wataarifa sahihi kwenye sekta hii utasaidi kuleta mageuzimakubwa kwenye kufanikisha azma ya nchi yetu kupiga hatuakwenye matumizi ya gesi za mitungi majumbani.

Mkurugenzi Mkuu wa TZLPGA, Amos Jackson akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye mjadala huo.

Kwa hiyo uwepo wenu hapa utasaidia sana kupanua ufahamu wetukupitia maoni yenu kama wadau muhimu wa sekta hii’.

Amos alisema kuhusu mikakati iliyowekwa na umoja huo, alisema, ‘tumedhamiria kupanua matumizi ya teknolojiahii ya gesi za majumbani katika katika kupunguza uzalishajiwa kaboni, kuboresha ufanisi wa nishati, na kurahisishamatumizi mbadala za nishati safi’.

Mwenyekiti wa TZLPGA, Benoit Araman akizungumza na wageni waalikwa kwenye mjadala huo (hawapo pichani)

Aidha, Mwenyekiti wa TZLPGA, Benoit Araman alisisita umuhimu wa kudumisha ushirikiano baina ya wadauwa sekta hio na serikali.

Alisema, ‘ni wajibu wetu kuiungamkono serikali kuhakikisha tunaleta mapinduzi kwenye sektahii ya gesi majumbani ili kutokomeza uharibifu wa mazingiraunatokokana na matumizi ya mkaa’.

Aliendelea, ‘mkaa nitishio kwa maana huchangia kutengeneza hewa ya kaboniambayo inachafua mazingira na kuleta mabadiliko hasi yatabia ya nchi’.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile

Mdhahalo huo uliohudhuriwa na mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Andilile ambae ameungamkono uzinduzi wa kampeni wa kusambaza taarifa sahihi juuya matumizi salama ya gesi (LPG) kwa manufaa ya taifa kwaujumla.

TZLPGA imeahidi kushirikiana na wadau wa sekta hio kutoamsukumo wa wawekezaji kutoa pesa kwa ajili ya kukuzamatumizi ya nishati safi na athari zingine chanyazitakazosaidia kuwa tija kwa sekta ya nishati kwa ajili yamaendeleo ya Taifa zima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Moduli ya kuwasilisha rufaa za zabuni kieletroniki kuanza Julai

Spread the loveMamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imesema moduli...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mshindi ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ akabidhiwa trekta

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imehitimisha msimu wa tatu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hati Fungani ya NMB Jamii yaanza kuuzwa Soko la Hisa London

Spread the loveBenki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya...

Biashara

Vuna mapene hadi Mil 400 ukicheza Expanse Tournament 

Spread the love  Promosheni ya kuvuna mahela ya Meridianbet bado inaendelea kusaka...

error: Content is protected !!