Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Nimempoteza rafiki hodari wa mabadiliko
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Nimempoteza rafiki hodari wa mabadiliko

Spread the love

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadem), Freeman Mbowe ameeleza kupokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema amepoteza rafiki, ndugu na mshauri mzuri lakini pia Tanzania na dunia imepoteza kiongozi shujaa, mwenye mchango mkubwa katika kujenga amani, ushirikiano na ustawi wa jamii.


Katika taarifa aliyoitoa kwa umma leo Jumapili, Mbowe amesema Lowassa alikuwa kiongozi shupavu, mwanasiasa mahiri, mwanaharakati hodari na alikuwa mstari wa mbele katika kupigania mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini mwetu.

“Alikuwa rafiki yangu na mshirika katika safari ya kuleta demokrasia ya kweli Tanzania. Alikuwa mtu mwenye hekima, busara, ujasiri, uzalendo, mtu mwenye huruma, upendo na msamaha kwa wote. Alikuwa mtu mwenye maono, mipango na mtekelezaji mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Kwa niaba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Watanzania wenzangu, napenda kutoa salamu zangu za dhati, za Pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wapenda demokrasia wote kwa kifo chake.

“Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, amsamehe makosa yake na amjaalie rehema zake. Mungu aipe faraja, nguvu na subira familia yake, chama chake, wafuasi wake na wote walioguswa na msiba huu,” amesema.

Amesema wataendelea kuenzi kazi, mawazo na hekima alizotuachia Mheshimiwa Lowassa. Pia wataendelea kumuombea na kumkumbuka kwa mema aliyotutendea.

“Mungu ailaze roho ya Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa mahali pema peponi. Amina,” amesema Mbowe.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!