Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Babu Duni amlilia Lowassa, akumbuka walivyoshinda uchaguzi 2015
Habari za Siasa

Babu Duni amlilia Lowassa, akumbuka walivyoshinda uchaguzi 2015

Spread the love

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Juma Duni Haji ‘Babu Duni’ ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 alikuwa Mgombea Mwenza wa Hayati Edward, amesema atamkumbukwa kwa mengi mwanasiasa huyo mkongwe ikiwamo namna alivyoiteka mioyo ya Watanzania  kwa kuwa mgombea mwenye kupendwa zaidi.  Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Babu Duni na Lowassa ambao waligombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Februari 2024 alipokuwa akizungumza na MwanaHALISI ONLINE jijini Dar es Salaam kuhusu kifo cha Waziri Mkuu huyo mstaafu.

“Tunachoweza kusema kuhusu Mzee Lowassa ni namna alivyokuwa akipendwa  na akakubalika na jamii ya Watanzania… kwamba yeye alikuwa tegemeo lao la  kuleta mabadiliko ya maisha na siasa nchini,” amesema.

Amesema kielelezo cha kupendwa kwa Hayati Lowasa ni ule  mkutano wao uliofanya Jangwani ambapo  ulikusanya watu wengi kiasi kuitwa mafuriko.

Amesema Lowasa hakuwa Rais kwa sababu ya mfumo mbaya wa siasa za Tanzania,  “Kwa kifupi kulikuwa na hakuna wa kuzuia Mzee yule kuwa Rais isipokuwa Mungu hakutaka na siasa zetu za Tanzania na kwa Taarifa za watu waliokuwa wanajua data za uchaguzi ule wanasema tulishinda “

Babu Duni anasema kuwa Hayati Lowasa alikuwa na roho ya kisultani ambayo ni roho ya ukarimu.

“ Alikuwa na huruma… alikuwa na mkono mwepesi kwa kweli kwetu maana yake hakuwa bahili wakutoa,” amesema.

Lowassa amefariki dunia jana Jumamosi wakati akipatiwa matibabu ya magonjwa ya utumbo kujikunja, mapafu ma shinikizo la damu katika Hospitali ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!