Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wabunge watoa mbinu za kuongeza mapendekezo yaliyoachwa kwenye Muswada wa Habari
Habari Mchanganyiko

Wabunge watoa mbinu za kuongeza mapendekezo yaliyoachwa kwenye Muswada wa Habari

Spread the love

 

WADAU wa Haki ya Kupata Habari (CoRI), wameshauriwa kuwasilisha hoja nzito zitakazoshawishi wabunge kuwasilisha bungeni maoni yao yaliyoachwa katika Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, ili yajumuishwe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wabunge kwa nyakati tofauti walipokuwa wanazungumza na ujumbe wa CoRI, jijini Dodoma.

Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile, amesema ujenzi wa hoja imara utashawishi wabunge kubeba maonni yao yaliyoachwa ili yajumuishwe katika Muswada huo.

“Muwe na ufafanuzi halisi unaoweza kushawishi wabunge tena kwa mifano. Mfano mnataka kusiwepo na leseni, je nchi nyingine zinafanyeje hasa za Afrika. Kila hoja mnayotoa iwe na ufafanuzi mzuri kwa wabunge, mkifanya hivyo mnaweza shawishi wabunge na jambo linaweza kuwa rahisi,” amesema Dk. Ndugulile.

Kwa upande wake Mbunge wa Mafinga, Cosato Chumi (CCM) amesema sheria za nchi zinapaswa kuendana na mabadiliko makubwa ya teknolojia, vinginevyo zinaweza kuwa hazitekelezeki.

Chumi ametoa kauli hiyo baada ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, alipoeleza madhara ya kuwa na sheria za habari zinazoshusha taswira ya nchi kimataifa.

“Kuna Sheria inayokataza kuingia kwa machapisho ya nje bila kuweka vigezo halisi, kuwa na sheria kama hii tena inayompa mwanya waziri kuamua kuzuia machapisho kwa namna anavyojisikia, kunaweza sababisha machapisho yenye umuhimu kutoka nje hata kama yana faida kuzuiwa,” amesema Balile.

Kwa upande wake Mbunge Viti Maalum, Nusrat Hanje (Chadema) amesema sheria hiyo ina kasoro katika kipengele cha utoaji leseni kinachoipa mamlaka Idara ya Habari (Maelezo), kuamua nini cha kufanya kwa chombo cha habari husika.

“Wakati mwingine Serikali inaweza kuamka na stress na ikaja na maamuzi ambayo sio, ni vizuri vyombo vya habari mambo yao yakawa yanafanyika kwenye bodi,” amesema Hanje na kuongeza:

“Ninaona hoja zenu na umuhimu wake, sisi kama wabunge tutashauri kamati namna bora ya kuliendea hili. Tunatakani kuwa na Sheria zinazoishi muda mrefu.”

Mbunge Viti Maalum, Judith Kapinga, amesema kwa ufafanuzi uliotolewa na CoRI unaonyesha baadhi ya maoni yaliyoachwa ni muhimu kujumuisha kwenye Sheria hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!