Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge wamkaanga Askofu Gwajima, Silaa
Habari za SiasaTangulizi

Wabunge wamkaanga Askofu Gwajima, Silaa

Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge Tanzania
Spread the love

 

SAA chache baada ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutoa azimio la kuwasimamisha mikutano miwili wabunge wa Askofu Josephat Gwajima (Kawe), Jerry Silaa (Kawe), baadhi ya wabunge wakiwamo wa CCM wamesema adhabu hiyo haitoshi. Anaripoti Gabriel Mushi, Dar es Salam … (endelea).

Wabunge hao wiki iliyopita waliitwa mbele ya kamati hiyo kwa kuhojiwa kuhusu matamshi waliyotoa nje ya Bunge.

Akiwasilisha taarifa ya uchunguzi wa kamati kuhusu tuhuma zinazowakabili wabunge hao, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka amelieleza Bunge kuwa wabunge hao walishindwa kuwasilisha ushahidi wa tuhuma walizozitoa dhidi ya mhimili huo.

Amesema wabunge hao mbali na adhabu walizopewa, lakini wanatakiwa kuangaliwa kuhusu mienendo yao nje ya Bunge.

MICHANGO YA WABUNGE

Baadhi ya wabunge waliochangia taarifa ya kamati hiyo, ni Mbunge Viti maalumu- Chadema, Tunza Issa Malopo ambaye pia ni Mjumbe Kamati hiyo, alisema kwa masikitiko makubwa Gwajima na Silaa hawakuwa na vielelezo vyovyote kuhusu tuhuma walizozitoa.

Alisema Gwajima alidai kuwa chanjo ya JJ imeletwa kwa sababu watu wamekula pesa, lakini pia chanjo hiyo inasababisha watu wanakuwa vichaa lakini walipomtaka alete ushahidi hakuwa nao.

Alisema hata walipomuuliza kwamba kwanini hakufuata utaratibu wa kutoa ushauri au kukosoa kwa sababu yeye ni mbunge wa CCM na kiongozi wake ndiye Rais, bado Gwajima alionesha ukaidi.

“Askofu Gwajima aliiambia Kamati kuwa yale aliyoyasema, atayasema akiwa ndani ya Bunge, atasema akiwa nje ya Bunge, atasema akiwa juu ya dari na atakayemsemesha atasema zaidi ya mara mbili.  Gwajima alituambia kamati kuwa ataendelea kusema. Kwa hiyo kazi kwenu wenye mamlaka.

“Ataendelea kusema… tusubiri jumapili inayokuja hatujui kitakachoenda kusemwa,” alisema Tunza.

Kauli ya Tunza iliungwa mkono na Mbunge wa Singida Magharibi (CCM), Elibariki Kingu ambaye alisema yeyote ambaye hajafurahia Rais

Samia Suluhu Hassan kuwepo madarakani au amechukia kwa kuwa hajapewa uwaziri, akae kimya kwani akileta chokochoko watamshughulikia.

“Rais Samia ana ushawishi mkubwa kwa wananchi na wanampenda sana, haijawahi kutokea kwenye nchi yetu fedha nyingi kiasi hiki zikapelekwa kwa wananchi.

“Tunakupongeza sana Spika kwa kusimama imara na kulinda heshima ya mhimili huu mara zote hujaacha Bunge lidhalilike,” alisema.

Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Kilumbe Ng’enda alisema kwa upande wake amejitoa kama dhabibu kumuonya Gwajima hivyo hata kama atamchapa kwenye madhabahu siku ya Jumapili, amchape ajuavyo lakini amuache Rais Samia afanye klazi.

“Mheshimiwa Spika, wabunge wengi ambao tumekutana huko nje tunazungumza juu ya tukio hili la mwenzetu (Gwajima), kila mmoja anasema kwakweli huyu bwana kafanya vibaya. Ukiwauliza mbona hamkemei wanasema tunaogopa, atapanda madhabahuni kwenda kutuchapa,” alisema Ng’enda.

Kuhusu tuhuma za Askofu Gwajima amepewa adhabu hiyo huku alitakiwa kuchunguzwa na vyombo vingine kutokana na kinachodaiwa ni uchochezi na upotoshaji.

ADHABU ZAO HIZI HAPA

Bunge ambalo limepitisha maazimio ya kamati hiyo, mbali na wawili hao kusimamishwa kuhudhuria mikutano miwili hadi Januari 2022, kwa upande wa Gwajima kamati ilipendekeza afikishwe mbele ya kamati ya chama chake CCM ili akahojiwe huko kuhusu mwenendo wake.

Pia vyombo vya dola vimchunguze kutokana na tuhuma zinazomhusu kuwa za jinai.

Aidha, Silaa kamati ilipendekeza asimamishwe mikutano miwili pamoja na kuvuliwa uwakilishi wa Bunge la Afrika (PAP) kwa madai anaweza kusema uongo huko.

KILICHOWAPONZA

Wawili hao kwa nyakati tofauti walituhumiwa kulidharau Bunge na kuchonganisha mhimili huo na Serikali pamoja na wananchi.

Askofu Gwajima alituhumiwa kwa kauli zake alizozitoa kanisani  kwake tarehe 25 Julai, 2021, tarehe 1, 8, 15 Agosti 2021 wakati akizungumzia kuhusua suala la chanjo ya Virusi vya Corona.

Wakati Silaa alikumbwa na mkasa huo kutokana na kauli yake kuwa wabunge hawalipi kodi katika mishahara yao jambo lililoelezwa ni uongo kwani wabunge wanalipa kodi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!