WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Askofu Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa (Ukonga), wamepewa adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge, baada ya kukutwa na hatia katika makosa ya kudharau na kudhalilisha mhimili huo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Adhabu hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 31 Agosti 2021, bungeni jijini Dodoma, baada ya wabunge kuunga mkono adhabu zilizopendekezwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, dhidi ya wabunge hao.
Akizungumza baada ya kuwahoji wabunge dhidi ya hoja ya kamati hiyo kuhisi adhabu ilizopendekeza dhidi ya wabunge hao, Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema adhabu hizo ni ndogo.
Na kwamba kama wataendelea kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu, watachukuliwa hatua zaidi.
“Bunge lote limeafiki kabisa adhabu zile na adhabu hizi zimetolewa kwa kweli ni ndogo sana, huo ni ukweli kwa makosa waliyotenda sababu ni mikutano miwili na maana yake huu unahesabika kiukweli wanakosa huo unaokuja. tunasikitika ni ndogo mnajua kanuni zinaruhusu kutoa adhabu nyingine zaidi ya hivyo. Tutakuwa tayari kufanya hivyo wakitulazimisha kufanya hivyo,” amesema Spika Ndugai.
Kwa mujibu wa Spika Ndugai, adhabu yao itaishia katika mkutano wa tano na wataanza kuhudhuria mkutano wa sita utakaoanza utakaoanza Januri 2022.
Awali, kamati hiyo ilipendekeza wabunge hao wasimamishwe kuhudhuria mikutano miwili na au mitatu mfululizo, baada ya kuwakuta na hatia walipohojiwa.
Leave a comment