Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia
Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeliagiza Shirika la Maendeleo ya petrol nchini (TPDC), kuongeza kasi ya kuunganisha wateja katika mfumo wa matumizi ya gesi asilia ili kupunguza na matumizi ya kuni na mkaa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … ( endelea).

Hayo yambainishwa jana Jumamosi wakati kamati hiyi ilipofanya ziara katika viwanda mbalimbali Jijini Dar es salaam ili kukagua miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia inayotumika katika Viwanda vinavyotumia mfumo wa gesi Asilia kama nishati.

Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake, Mathayo David Mathayo, ilitembelea kiwanda cha MMI STEEL TANPACK kinachojishughulisha na utengenezaji wa mabati kwa kutumia teknolojia ya gesi asilia kilichopo Jijini dar es salaam.

Ziara hiyo imefanyika kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa hapa nchini, na kujionea ufanisi wa utekelezaji wake na kuuponheza uongozi wa kiwanda hicho kwa kutumia teknolojia ya gesi asilia, na kuwataka watanzania kutumia gesi asilia katika shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. James Mataragio amesema Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya petrol nchini ( TPDC), inaendelea na kazi mbalimbali za kuunganishia wateja wapya gesi asilia ikiwemo viwandani pamoja na hoteli, ili kuendelea kukuza matumizi ya nisha hiyo.

“Gesi asilia inatumika viwandani na majumbani, hivyo tunawakaribisha wawekezaji wanaohitaji matumizi ya gesi kwa ajili ya uzalishaji na shughuli za kibiashara kujitokeza kwakuwa miundombinu ya gesi ipo tayari” amesema Mataragio.

Ziara hiyo imehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, Mussa Makame na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na TPDC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!