Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vyama vya siasa vyaomba Chadema ifutwe, msajili atoa kauli
Habari za SiasaTangulizi

Vyama vya siasa vyaomba Chadema ifutwe, msajili atoa kauli

Ofisi ya Chadema Makao Makuu, Dar es Salaam
Spread the love

BAADHI ya vyama vya siasa vya upinzani nchini vimeitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, ivifutie usajili vyama vinavyokiuka sheria katika ufanyaji mikutano ya hadhara, kwa kutoa lugha za kuchochea ubaguzi, udini na kejeli dhidi ya viongozi wa Serikali. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumanne, tarehe 1 Agosti 2023, jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa dharura ulioitishwa na Baraza la Vyama vya Siasa nchini kwa ajili ya kujadili hali ya kisiasa ambao umeshirikisha viongozi wa kisiasa na kidini.

Miongoni mwa vyama vinavyotuhumiwa kutumia mikutano ya hadhara kutoa lugha zisizo na staha dhidi ya viongozi wa Serikali, hususan wakati wanawasilisha hoja zao kuhusu sakata la uwekezaji bandari ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo makamu Mwenyekiti wake Bara, Tundu Lissu, ametakiwa kuripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), kujibu tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK), David Mwajojele, amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kufuta usajili wa vyama hivyo.

“Sheria inasemaje kikundi cha dini au chama cha siasa kinachotamka maneno mabaya na matusi? Sasa hili suala kama mara ngapi nasikia mtu huyohuyo anaongea maneno haya huyu apewe adhabu. Napendekeza hjawa jamaa wachukuliwe hatua wasirudie tena au wafute chama hicho sababu kinakiuka sheria,” amesema Mwaijojele.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Ali Omary Juma, amelitaka Jeshi la Polisi nchini, kuwashughulikia watu wanaotoa kugha za matusi katika mikutano ya hadhara.

“Katika mikutano ya hadhara kuwe na sheria ya kuiwaadhibu wanaomtukana Rais, Jeshi la Polisi lipewe mamlaka hayo kwamba sasa matusi basi. Leo anasimama mwanmasiasa anasema uzanzibar na kuligawa taifa, tukiacha hivi tunakoelekea kubaya,” amesema Juma.

Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Richard Lyimo, amesema “hatua zichukuliwe sababu tunawafundisha watoto wetu vitu vibaya, wanafundisha matusi badala ya maadili mema. Kuna haja ya kuondoa siasa kwenye masuala yanayohusu jamii.”

Dk. Avemaria Semakafu amevitaka vyama vya siasa kuanzisha program za kuwafundisha wafuasi wake hasa vijana, kujenga hoja badala ya kutumia matusi ili kuungwa mkono.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Mvita Mustafa Ali, amechangia mjadala huo akisema “kwenye mada inayosema kumetyokea wimbi la lugha chafu wanasimama kwenye majukwaa wanatoa maneno hatarishi na pia tunakwenda mitandaoni unakuta lkugha chafu. Kama kunawezekana haya mambo yakatazamwa upya, matusi na kejeli zinatuvunja moyo kiongozi wangu (Rais Samia) atakuwa katika hali gani?

Naye  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prpof. Ibrahim Lipumba, amewataka wanasiasa kuacha kutoa lugha zinazochechea udini na ubaguzi, pamoja na kuhatarisha muungano.

“Sababu wanakutana naye (Rais Samia) kirahisi, sasa inaweza kuwa sababu hiyo. Unaweza kuwa na hoja zako nzuri za DP World ukazileta bila kusema wazanzibar ndiyo uwasilishe, kulikuwa na mijadala ya ufisadi hapakuwa na mzanzibar hata mmoja,” amesema Prof. Lipumba.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema changamoto ya utoaji lugha zisizo na maadili katika mikutano ya hadhara, inachochea na kitendo cha Serikali kuchelewesha marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, kwani kama ingekamilisha zoezi hilo kamati ya maadili ingeanzishwa kwa ajili ya kushughulikia wanaozitoa.

“Kinachochelewesha utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi ni nini? Sheria zikirekebishwa kutakuwa na kanuni za maadili mtu akionekana ametukana ataenda kamati ya maadili na adhabu zitatolewa . Ofisi ya msajili mnasababisha haya yaliyoko sasa, pelekeni muswada bungeni na haya yote mtayapatia majibu,” amesema Zitto.

Akijibu maombi hayo, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amesema kazi yake ni kulea vyama vya siasa na si kufuta usajili wake na kwamba wameitisha mkutano huo wa dharura kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizojitokeza.

Jaji Mutungi amesema kuwa, kama ofisi yake itachukua jukumu la kufuta chama cha siasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi italeta tmalalamiko yasiyokuwa na sababu za msingi.

“Ukisema msajili hujatoa adhabu, ninachotaka kusema tunakuja kukaa hapa kujibu tatizo la matatizo ya huyu mnayemuongelea. Wanasiasa mnajijua vingine vinakwenda kama chambo, utakuta tatizo moja linaibua linguine,” amesema Jaji Mutungi.

Msajili huyo wa vyama vya siasa, amewataka watu wenye malalamiko kuhusu suala hilo, iyawasilishe ndani ya Kamati ya Maadili ya Baraza la Vyama vya Siasa kwa ajili ya kufanyiwa kazi “isije ofisi ikaonekana inaonea chama wakati tunaelekea kwenye uchaguzi, kama kuna vitu vya kuelekzana nasema mi sina mahakama, mimi ni mlezi wa vyama .”

Mkutano huo ulishirikisha vyama mbalimbali, ambapo Chadema hakikushiriki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!