Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mpango aanika mikakati kuimarisha sekta ya kilimo
Habari Mchanganyiko

Dk. Mpango aanika mikakati kuimarisha sekta ya kilimo

Kilimo cha parachichi
Spread the love

MAKAMU wa Rais nchini Dk. Philip Mpango ameweka wazi mipango ya serikali ya kuimarisha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuongeza thamani mazao na kipato kwa wakulima wafugaji na wavuvi. Anaripoti Isaya Temu, Tudarco …(endelea).

Hayo ameyasema leo tarehe 1 Agosti 2023 wakati wa uzinduzi maonyesho ya kimataifa ya wakulima Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Dk. Mpango amesema kufanya hivyo ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 “Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya kilimo,  mifugo na uvuvi ili kuongeza uzalishaji, tija na thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na kukuza kipato na kutoa ajira kwa wananchi”.

Dk. Mpango amebainisha dhamira ya serikali katika kuinua sekta ya kilimo kwa kuongeza  bajeti ya mwaka 2023/2024.

Amesema kuwa Serikali imeiongezea bajeti wizara kwa asilimia 330 ambapo kwenye sekta ya uvuvi na mifugo serikali imetenga bilioni 295 kwa mwaka 2023/2024 kutoka Bilioni 275 mwaka 2021/2022.

Ameeleza kuwa bajeti ya Sekta ya kilimo  imepanda kutoka bilioni 294 kwa mwaka 2021/2022 hadi bilioni 978 mwaka 2023/24.

“Hii itasaidia katika kuimarisha maeneo ya utafiti na huduma za ughani, kutoa ruzuku ya pembejeo za kilimo, ufugaji na uvuvi, kuimarisha upatikanaji wa mitaji, kuimarisha miundombinu ya uhifadhi wa mazao, kuanzisha na kuhamasisha mashamba makubwa ya  pamoja, na kuimarisha maendeleo ya ushirika”amesema Dk. Mpango.

Dk. Mpango ametoa wito kwa wizara kujiandaa kuratibu shughuli za Jukwaa la Chakula Afrika kwa kuwa  kuwa Tanzania imekuwa mwenyeji wa jukwaa hilo litakalofanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Katika uzinduzi wa maonesho hayo Waziri wa Kilimo, ufugaji na uvuvi, Hussein Bashe amemuomba Dk. Mpango kuwapa zawadi ya Tuzo na fedha  kwa watafiti mbalimbali waliogundua mbegu bora za kilimo ambazo zinastahimili ukame na kutoa mazao mengi na bora.

Waziri Bashe hajaishia hapo amesema kuwa watafiti hao watajengewa nyumba za kisasa na Wizara ya Kilimo katika viwanja vilivyopo katika eneo lolote ambalo watafiti hao watachagua.

Watafiti hao ni pamoja na Dk. Zubeda Nduruma aliyegundua mbegu ya Mahindi, Crescensia Rutaiwa aliyegundua mbegu ya alizeti iliyoitwa Record.

Zakaria Kanyeka akiwa pamoja na Maulid Penza waliogundua mbegu ya Mpunga na Dk Atugonza Bilaro aliyegundua mbegu ya mahindi inayoitwa Tumbi 105.

Waziri Bashe amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa kuvifanya viwanja vyote vinavyotumika kwa ajili ya maonesho ya Kilimo Nane nane Tanzania kuwa na viwango vya kimataifa .

Viwanja hivyo ni pamoja na kiwanja cha Nane nane Mbeya na Dodoma.

Maonesho yam waka huu yamechagizwa na kauli mbiu isimayo ‘Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu wa chakula’.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA yatekeleza agizo la Samia kwa kutangaza zabuni kielektroniki

Spread the loveKiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava...

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

error: Content is protected !!