Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais awatimua mawaziri kwa kuchelewa kikaoni
KimataifaTangulizi

Rais awatimua mawaziri kwa kuchelewa kikaoni

Dk. Wiliam Ruto
Spread the love

RAIS wa Kenya, William Ruto amemtimua Waziri wa Biashara, Moses Kuria na mwenzake wa Usalama wa Ndani Kithuri Kindiki baada ya kuchelewa kwenye hafla ya utiaji saini mikataba ya zabuni mbalimbali iliyofanyika ikulu jijini Nairobi. Anaripoti Mlelwa Kiwale, Tudarco … (endelea).  

Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 1 Agosti 2023, ambapo imeelezwa kuwa  Rais Ruto aliwahi kufika kwenye ukumbi uliopangwa kufanyika shughuli hiyo kabla ya mawaziri hao ndipo alipoamua kufunga mlango.

Kiongozi huyo mkuu wa Kenya amesema mawaziri hao watalazimika kujieleza juu ya kitendo hicho kwa njia ya maandishi.

 “Kwa hiyo wale ambao waliochelewa ambao ni watumishi na watendaji waandamizi, nategemea kupata maelezo kwa maandishi.  Licha ya kudai kuwa wamechelewa sababu ya foleni nataka kufahamu kwanini hawaichukulii hii hafla ya utiaji saini mikataba kwa umakini”.

Aidha, Rais Ruto ametoa tahadhari kwa watumishi wengine wa umma kuacha kubeza shughuli hizo kwa kuona kuwa hazina msingi kwenye utendaji serikali.

Ruto alionesha kukasirishwa na kusema kuwa inaonekana wafanyakazi wa serikali yake wanaichukulia hafla hiyo kama  ibada.

“Sijajua kwamba sababu ya hii usainishaji wa mikataba uliokuwa ukiendendelea takribani miaka 20 sasa watu wanafikiria kwamba ni ibada”

“Ndiyo maana watu wanachukulia kama kitu cha zamani na kuleta samahani zisizo za maana” amesisitiza Ruto.

Ruto amesema mtumishi wa  serikali ambaye hakuzingatia muda anatakiwa kujiuzulu mwenyewe.

“Kama hautoweza kuzingatia muda kwa muajiri wako, basi unatakiwa kujiuzulu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

error: Content is protected !!