Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uvumilivu wamshinda Mbowe, aivaa familia ya Lowassa
Habari za SiasaTangulizi

Uvumilivu wamshinda Mbowe, aivaa familia ya Lowassa

Freeman Mbowe, Mwenykiti wa Chadema
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza kusikitishwa na hatua ya familia ya Hayati Edward Lowassa kuandika historia ya waziri mkuu huyo mstaafu wa Tanzania bila kuitaja Chadema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Mbowe ambaye leo Ijumaa amekaribishwa kutoa salamu za rambirambi licha ya kwamba itifaki hiyo haikupangwa kwenye ratiba rasmi iliyotolewa na kamati ya mazishi, alianza kuwa kusisitiza kuwa anaweka rekodi sawa.

“Huwezi kuandika historia ya Lowassa ukaacha neno Chadema. Nimesikiliza na kusoma sana historia ya Lowassa… binafsi nimesikitika,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema Lowassa ambaye amezikwa nyumbani kwao katika kijiji cha Ngarash wilayani Monduli mkoani Arusha, amefanya mambo mengi makubwa ndani ya Serikali, CCM na katika vyama vya upinzani.

Amesema ni jambo ambalo haliwezekani kuzungumzia historia ya Mbowe bila kuitaja Chadema ambayo alikuwa mtumishi wake kwa miaka minne katika nafasi ya mjumbe wa kamati kuu Chadema na mgombea urais ambaye alijenga demokrasia ambayo halijawahi kufikiwa.

Mbowe amesisitiza kuwa Lowassa alikuwa mtu wa karama kwa sababu pamoja na sifa nyingi alizopewa ila ni dhahiri alikuwa mtu wa karama ya ajabu.

“Aliweza kuunganisha makundi mbalimbali wakati wote. Wenzangu CCM na serikali alianza safari ya matumaini kisha akahamia safari ya mabadiliko Chadema… alileta kasi ya demokrasia katika nchi yetu.

“Aliwezesha kupatikana kwa wabunge 114 kutoka vyama vya upinzani. Madiwani zaidi ya 2000 karibu nusu ambayo ni karibu nusu ya kata za Tanzania bara. Vyama vingine vya upinzani vikaongoza majiji katika jiji la Dar es Salaam, Mbeya na Arusha hivyo hampaswi kupuuza historia hii viongozi wangu,” amesisitiza Mbowe na kupigiwa makofi na waombolezaji.

Amesema kwa miaka minne Lowassa alitoa mchango mkubwa kwa upinzani hasa ikizingatiwa alikuwa mnyenyekevu kwa yeyote aliyefanya naye kazi kwani kila mmoja yake aliishia kuwa rafiki yake.

“Alikuwa hana mipaka ya kikabila na kiimani alimfanya kila mtu kuwa ndugu yake,” amesema Mbowe.
Pamoja na mambo mengine, Mbowe amemshukuru mke wa marehemu, Regina Lowassa kwa kumpokea vizuri alipokwenda kumjulia hali waziri mkuu huyo alipokiwa akitibiwa Afrika Kusini.

Pia amemshukuru kwa kuwa na moyo wa upendo alipotoa mchango wa kutafuta madaktari kumtibu mtoto wa familia ya Mbowe aliyetakiwa kuelekea katika hospitali aliyokuwa akitibiwa Lowassa Afrika kusini lakini bahati mbaya alifariki kabla ya kupelekwa katika nchi hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Mbowe amesisitiza kuwa Lowassa alikuwa mhanga wa mifumo mibovu ya uchaguzi.

Familia ya Hayati Edward Lowassa

“Ni mgombea urais aliyepata kura zaidi ya milioni sita. Alikuwa ni full potential (uwezo) ya kuwa kiongoza lakini potential ya Lowassa haikuwahi kutumika hivyo tuwape watu nafasi,” alimaliza Mbowe na kushangiliwa kwa nguvu.

Lowassa ambaye amefariki dunia tarehe 10 Februari mwaka huu, alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Lowassa alihamia Chadema baada ya CCM kumuengua katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea urais wa chama hicho nafasi ambayo alipewa Dk. John Magufuli.

Hata hivyo, mwaka 2019 Lowassa alirejea CCM hadi umauti unamfika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

error: Content is protected !!