Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Utafiti uboreshaji wa usafiri wa reli mijini kuanza jijini Dar
Habari Mchanganyiko

Utafiti uboreshaji wa usafiri wa reli mijini kuanza jijini Dar

Spread the love

 

SHIRIKA la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA) kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Shirika la Reli Tanzania (TRC) wamekubaliana kutekeleza mradi wa utafiti wa ukusanyaji wa data na uboreshaji wa usafiri wa treni za abiria jijini Dar es Salaam kuanzia mwezi huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayoa yamebainishwa mwishoni mwa wiki katika mkutano wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Utafiti huo wa miezi minne unaotarajia kukamilika Februari 2022, utachunguza miundombinu ya reli za abiria zilizopo Dar es Salaam (reli ya Pugu na Ubungo) na kupendekeza hatua mbalimbali za kuboresha miundombinu hiyo.

Mkutano huo uliohudhuriwa na washiriki 18 kutoka Ofisi ya JICA Tanzania, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, TRC na Washauri kutoka Japani na Tanzania walipendekeza mpango wa uboreshaji wa ufuatiliaji wa uendeshaji wa reli, uwekaji ishara, usafirishaji wa bidhaa, ujenzi wa stesheni katika vituo, majengo ya biashara katika stesheni na namna bora ya kutoa huduma ya usafiri katika njia za treni za abiria zilizopo.

Timu ya watafiti iliyoundwa, itajadiliana na maofisa wa serikali ya Tanzania ili kurekebisha Mpango Kabambe wa Usafiri wa Mijini wa Dar es Salaam wa mwaka 2018, ambao ulifadhiliwa na JICA.

Mpango huo kabambe unakadiria kwamba Dar es Salaam itakuwa na zaidi ya watu milioni 10 mapema mwaka 2030, hivyo usafiri wa barabara pekee hautaweza kutoa usafiri wa uhakika na kuondoa kero ya msongamano wa magari (foleni) na kutumia muda mrefu wa kusafiri ndani ya jiji hilo.

Mkutano huo pia ulipendekeza namna bora ya uboreshaji wa mfumo wa reli uliopo kwa ajili ya maendeleo ya usafiri na mipangilio mizuri yenye uwiano.

Mikutano zaidi ya majadiliano itaendelea  kufanyika  kila inapohitajika, hadi kukamilika kwa utafiti  huo mnamo Februari 2022.

Shirika la Maendeleo la  Kimaitaifa la Japani (JICA) limekuwa likisaidia sekta ya uchukuzi kwa zaidi ya miaka 40 hapa Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!