Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msajili ailima barua NCCR-Mageuzi, yamjibu na kusema…
Habari za Siasa

Msajili ailima barua NCCR-Mageuzi, yamjibu na kusema…

Jaji Francis Mungi, Msajili wa Vyama vya Siasa
Spread the love

 

MVUTANO kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania na Chama cha NCCR-Mageuzi umeanza upya, hivyo ndivyo unaweza kusema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Hivi karibuni ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilitangaza kuandaa kikao kitakachoshirikisha wadau wa siasa ili kupata ufumbuzi wa malalamiko ambayo yalitolewa na vyama vya siasa, kikiwemo NCCR-Mageuzi kuwa Jeshi la Polisi linavunja Sheria ya Vyama vya Siasa.

Baada ya kutangaza kikao hicho, vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na ACT-Wazalendo vilitangaza kutoshiriki, hali ambayo inatajwa kusababisha kikao hicho kuahirishwa.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa 21 Oktoba 2021, iliandika barua yenye Kumb. Na. HA. 322/362/18/11, ikitaka chama hicho kuwasilisha maelezo ambapo Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa chama hicho, Edward Simbeye alisema wanaona barua hiyo inauhusiano na msimamo wao.

Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo imeandikwa na Naibu Msajili, Sisty Nyahoza, ilisema wamepokea malalamiko kutoka kwa mwanachama wa chama hicho, Yeremia Maganja akieleza kuwa, uchaguzi wa Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara na Wajumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho uliofanyika 16 Januari 2021, haukufuata utaratibu ulioelezwa katika Katiba na Kanuni za chama chao, hivyo ni batili.

Undani wa habari hii, kujua barua husika na majibu ya NCCR- Mageuzi kwenda kwa msajilim soma Gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Jumatatu tarehe 8 Novemba 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!