Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ushirikiano NMB Foundation, NGO’s kunufaisha Watanzania
Habari Mchanganyiko

Ushirikiano NMB Foundation, NGO’s kunufaisha Watanzania

Spread the love

NMB Foundation imesaini makubaliano ya kushirikiana na asasi mbili kubwa za kiraia nchini yenye lengo la kuendeleza ustawi wa jamii na kutekeleza mipango chanya ya uwezeshaji kijamii na kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu….(endelea).

Utiaji wa saini za makubaliano hayo na taasisi za Legal Services Facility (LSF) na ile ya Benjamin Mkapa Foundation umefanyika wiki hii jijini Dar es Salaam kwenye Makao Makuu ya Benki ya NMB zilipo ofisi za NMB Foundation.

Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya (wa pili kushoto) wakibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo katika kuboresha huduma za afya, elimu na kuwawezesha vijana na wanawake. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam jana Alhamisi. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mashirikiano wa Mkapa Foundation, Mariam Ndabagenga na kulia ni Meneja Mwandamizi NMB Foundation, Vallerian Fernandos.

Akizungumza wakati wa matukio hayo, Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna alisema ushirikiano huo ni sehemu ya kutimiza dhamira ya taasisi hiyo ya kushirikiana kimkakati na wadau mbalimbali wa maendeleo na kuwekeza kusaidia kuboresha maisha ya wananchi.

Makubaliano kati ya NMB Foundation  na LSF yanayolenga hasa kuwainua wanawake na wasichana kijamii na kiuchumi yalisainiwa juzi Jumatano.

Kupitia ushirikiano huo, washirika hao watayasaidia pia makundi mengine yaliyosahaulika na yenye uhitaji katika jamii.

Makubaliano ya kufanya kazi na Taasisi ya Mkapa Foundation yalisainiwa siku iliyofuata (Alhamisi) yakilenga hasa kutekeleza miradi ya kijamii ya maendeleo yenye tija hususani kuziimarisha huduma za elimu na afya kupitia programu endelevu.

Karumuna alisema ingawa dhamira yao ni kuwa na ushirikiano wa muda mrefu wenye tija na matokeo chanya ya kijamii na kiuchumi, mikataba hiyo miwili itaanza kutekelezwa kwanza mwa muda wa miaka mitatu.

Aidha, alibainisha kuwa ushirikiano na LSF utajikita zaidi katika maeneo ya kipaumbele kiutendaji kwa mashirika hayo ambayo ni elimu, afya, mazingira na ujasiriamali.

“Kama taasisi inayotekeleza miradi ya kijamii, NMB Foundation inategemea makubwa sana kutokana na ushirikiano huu. Haya ni makubaliano kati ya taasisi mbili zenye ushawishi katika maeneo yake ya kiutendaji, ambayo tunaamini kwa dhati kuwa yatakuwa na manufaa makubwa kwa jamii zetu,” amesema Karumuna

Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala amesema ushirikiano huo ni mfano mzuri wa jinsi sekta binafsi na asasi za kiraia zinavyoweza kushirikiana kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

Kiongozi huyo alisema makubaliano hayo pia yanazipa fursa NMB Foundation na LSF kutoa mchango wenye tija katika juhudi za kutokomeza umaskini, kuondoa tofauti za kijinsia katika jamii na kukuza ukuaji jumuishi wa uchumi.

Mbali na utoaji wa ushauri wa kitaalam katika kubuni na usimamizi wa miradi yenye nia ya kuimarisha afya na elimu nchini, ushirikiano wa NMB Foundation na BMF unalenga pia kuimarisha na kutekeleza afua za mabadiliko ya tabianchi na athari zake hasa kwa afya za watu.

Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya (wa pili kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo katika kuboresha huduma za afya, elimu na kuwawezesha vijana na wanawake. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Mashirikiano wa Mkapa Foundation, Mariam Ndabagenga na kulia ni Meneja Mwandamizi NMB Foundation, Vallerian Fernandos.

Vile vile taasisi hizo zitajikita kuwasaidia na kuwawezesha vijana na wanawake kujikwamua kiuchumi kwa njia ya ubunifu na teknolojia wakiwemo wale wanaojishughulisha na ukulima wa mwani.

Wakizungumza kabla ya utiaji saini wa ushirika wao, viongozi wa NMB Foundation na BMF walisema watatumia zaidi uzoefu na utalaamu wa taasisi zao kuhakikisha malengo ya kushirikiana yanafanikiwa kikamilifu na kuwa na tija stahiki kwa jamii.

“Sisi tupo zaidi katika sekta ya kifedha na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation ni nguli katika eneo la afya na elimu ikiwa na historia ya mafanikio makubwa. Hivyo ni mategemeo yetu kuwa kuunganishwa kwa nguvu zetu kwa pamoja kutawezesha miradi mingi kuanzishwa na kuwafikia Watanzania wengi zaidi Tanzania Bara na Zanzibar,” amesema Karumuna a

Aliongeza kuwa ushrikiano na BMF ni fursa kwa asasi hizo kuongeza thamani katika jitihada za taifa kuboresha utoaji huduma za kijamii and kusaidia ukuaji endelevu.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa Foundation, Dk Ellen Mkondya-Senkoro, alisema vile vile wanalenga kuunganisha nguvu kutafuta pia rasilimali fedha ili kufikia malengo ya ushirikiano wao.

“Sekta za afya na elimu nchini ni maeneo muhimu kwa maendeleo ya jamii. Sisi kama Benjamin Mkapa Foundation, kwa miaka 18 sasa tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za serikali kuiimarisha hasa sekta ya afya,” kiongozi huyo alifafanua na kuongeza kuwa mchango wao na wadau wengine umekuwa na tija kubwa katika eneo hilo.

“Ushirikiano wetu na NMB Foundation utaongeza thamani kubwa katika hilo kutokana na uzoefu na utaalamu tulionao,” Dr Senkoro alisisitiza na kusema kuwa kufanyakazi pamoja kwa asasi hizo vile vile kunalenga kuwaongezea wataalam wa afya elimu, stadi na ujuzi, na pia fursa za ajira ndani na nje ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!