Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ushindi wa mpinzani Senegal wakoleza moto kwa wapinzani Tanzania
Habari za Siasa

Ushindi wa mpinzani Senegal wakoleza moto kwa wapinzani Tanzania

Spread the love

USHINDI wa aliyekuwa mgombea  urais wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ambaye amevunja rekodi ya kuwa Rais mwenye umri mdogo zaidi barani Afrika, umeacha somo kwa wanasiasa wa upinzani Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Faye mwenye umri wa miaka 44, alitangazwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni baada ya kupata asilimia 53.7 ya kura zilizopigwa, huku mgombea wa chama tawala nchini humo, Amadou Ba (62) akimbulia asilimia 36.2.

John Mnyika

Akizungumzia uchaguzi huo, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amesema mapambano yamemwezesha Faye kushinda kinyang’anyiro hicho ikiwa ni muda mfupi tangu aachwe huru kutoka gerezani alikokuwa anashikiliwa kwa makosa ya kisiasa.

“Novemba 2023 nilikuwa Senegal kama sehemu ya ujumbe wa kutaka kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko ambaye pamoja na mwenzake Faye waachiwe huru.

“Pia tulitaka chama chao cha PASTEF ambacho wakati huo kimefutwa na Serikali kirejeshwe na wote wapewe haki ya kushiriki uchaguzi wa 2024. Nilichobaini yalikuwepo mapambano toka wakati wa Rais Macky Sally alipoonyesha mwelekeo wa kutaka kugombea muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo,” amesema Mnyika.

Mnyika amesema kuwa, ushindi huo umetokana na ushirikiano wa kweli kati ya Sonko na Faye, pamoja na mapambano yaliyofanywa na wananchi kupitia njia mbalimbali ikiwemo kufanya maandamano kupinga hatua ya Rais wa zamani wa taifa hilo, Sally kutaka kuvunja katiba kwa kuongeza muda wa kukaa madarakani.

“Nimeshuhudia nguvu ya pamoja ya wawili hawa, sio tu katika mabango bali katika vituo vya kupigia kura nilivyotembelea jana asubuhi mpaka wakati wa matokeo jioni. Mapambano yameshinda Senegal, ni vyema nchi hiyo sasa ikajifunza kwenye mapitio ya marais wake na kizazi kipya kilete mabadiliko kwenye maisha ya watu,” amesema Mnyika na kuongeza:

“Kwetu Tanzania tuendeleze mapambano ya kikatiba na kisheria kuwezesha chaguzi huru na haki. Tujiandae kwa wiki ya maandamano tarehe 22 hadi 28 Aprili 2024.”

Kwa upande wake kiongozi wa zamani wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema nchi ya Senegal ni ya mfano wa kuigwa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter akimjibu Sakiete Kindunda aliyehoji kama Tanzania inaweza kutangaza matokeo mapema na kwa uwazi  kama Senegal ilivyofanya, Zitto alimjibu akisema hata wao wanaweza.

“Hata sisi tunaweza kupata Matokeo ndani ya masaa 6 baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa,” amesema Zitto.

Naye Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa, alisema “tumeamua, tumedhamiria, jiandaeni tunakuja.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!