December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Upinzani unabanwa, serikali iache upumue’

Spread the love

HASHIM Rungwe, Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA)-Taifa, amelalamika kwamba, serikali inavibana vyama vya upinzani nchini. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Anasema, ni wakati sasa kwa serikali kuacha vyama hivyo vipumue na vifanye kazi ya siasa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Aprili 2019 jijini Dar es Salaam katika mkutano mkuu wa pili wa chama hicho akisisitiza kwamba, uhuru wa upinzani ni sehemu ya amani ya nchi.

Mbele ya waandishi wa habari, siasa ni ya upinzani ni sehemu ya maisha ya binadamu na ni jukwaa pekee la wananchi kutoa maduku duku yao kuhusu mambo yanayoendelea nchini.

“Jukumu letu tufanya siasa, waache kuzuia zuia siasa sabahu ni maisha ya binadamu. Kuzuia mnawafanya wakose mahali pa kutoa maduku duku yao.

“Tunaiomba serikali iruhusu watu wafanye siasa kama ilivyokuwa zamani, wawe na mahali pa kutolewa dukuduku lao sasa hivi wamebanwa,” amesema Rungwe.

Katika hatua nyingine, Rungwe amevitaka vyombo vya dola kutozuia vyama hivyo kufanya mikutano ya kisiasa kwa kigezo cha uwepo wa viashiria vya uhalifu, akisema kwamba jukumu lao ni kulinda na si kuzuia.

“Sasa polisi walitakiwa waje watulinde, tunatakiwa tulindwe chama chochote kikitaka kufanya siasa barabarani, tunatakiwa tulindwe,” amesema Rungwe.

Mohammed Rashid, Makamu Mwenyekiti wa CHAUMMA wakati akihutubia kwenye mkutano  huo amesema, uvumilivu na ustahimilivu wa vyama vya upinzani katika muenendo wa demokrasia ndio chanzo cha amani ya taifa hili kudumu.

Rashid amewatala viongozi na wafuasi wa CHAUMMA pamoja na wa vyama vingine vya siasa nchini kutokuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

“Wapinzani ndio wanaoweka amani nchi hii, si wengine wowote,Huko vijijini mnakogombea kuweni wa kwanza kusimamaia Amani, haiwezekani mimi kiongozi wa taifa niwahamasisheni kufanya vita wakati mimi niko salama si vyema, sasa kama kuna watu wanahamasisha fujo itakuwa sio haki. Na watakaovunja sheria, kanuni ziansema wapi watapelekwa.kote pale tuahubiri Amani, “ amesema Rashid.

error: Content is protected !!