April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Njooni mnunue korosho-Serikali

Spread the love

WIZARA ya Viwanda na Biashara kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), imewataka wafanyabiashara, taasisi za umma na binafsi kujitokeza kununua korosho ghafi na zilizobanguliwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 6 Aprili 2019 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TanTrade, Theresa Chambo, zoezi la uuzaji wa korosho hizo bado linaendelea.
Taarifa hiyo imewataka watu wenye nia ya kununua korosho ghafi na zilizobanguliwa kuwasilisha maombi ya katika mamlaka ya TanTrade, ikiwemo taarifa za kiasi cha korosho wanazohitaji.

“TanTrade inapenda kuwafahamisha kuwa, zoezi la uuzaji korosho linaendelea. Hivyo wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda, hoteli, maduka ya jumla na rejareja, taasisi za umma na binafsi na wananchi kwa ujumla wenye nia ya kununua korosho wanakaribishwa kuwasilisha mahitaji yao,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

error: Content is protected !!