Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Upigaji wa kutisha ujenzi wa meli 5, mkandarasi ni dalali
Habari

Upigaji wa kutisha ujenzi wa meli 5, mkandarasi ni dalali

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameanika ubadhirifu wa kutisha katika mikataba ya ujenzi wa meli tano za Kampuni za kuhudumia Meli Tanzania (MSCL) na Mkandarasi YUTAKE kutoka nchini Uturuki. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Akizungumza leo Jumamosi tarehe 4 Disemba, 2021 wakati akizindua gati katika Bandari ya Dar es Salaam, Rais Samia ameeleza kusikitishwa na Watanzania ambao wameshiriki katika ubadhirifu huo.

Amesema jitihada za serikali katika kuimarisha usafiri na usafirisha kwa njia ya maji zinakwamishwa na makundi yaliyomo ndani ya serikali.

Amesema katika kufuatilia utekelezaji wa ujenzi wa meli hizo, amebaini kuwa ndani ya mkataba huo mkandarasi ana mtu anaitwa ‘wakala’ aliyepo Tanzania ambaye anatakiwa kulipwa dola milioni mbili kwa kila meli itakayojenga.

Amesema meli ya chini ilikuwa alipwe dola Marekani milioni milioni 1.9 pamoja na malipo madogo madogo.

“Nikaomba mkataba wa wakala nikaupata, kazi za wakala ni kufuatilia tenda zitakazotoka Tanzania, kuomba hiyo tenda  kujaza document za tenda… ni operational lakini wakala analipwa kwa kila meli itakayotengenezwa Tanzania kuanzia dola milioni 1.9 hadi mbili .

“Nikachukua hatua za kuagiza vyombo vya dola wamtafute wakala waongee naye, lakini nikamuita mkandarasi aliyeshinda hii tenda, mwishowe kaomba radhi na kukubali kuachana na wakala.

“Katika matayarisho ya kumfuatilia mkandarasi aliyepewa kujenga meli hizo, matayarisho yake yalikuwa yanatia wasiwasi na hakuonekana kama yupo tayari kujenga meli hizo,” ameeleza Rais Samia.

Kutokana na wasiwasi huo, Rais Samia amesema Serikali iliamua kuunda timu ya watalaam kutoka sekta mbalimbali; wizara ya ujenzi, wakili mkuu wa serikali, kampuni ya huduma za meli, jeshini kitengo cha Navy.

Ambapo timu aliiagiza kuelekea Uturuki kufuatilia hadhi au hali ya mkandarasi aliyeshinda tenda hiyo ya ujenzi wa meli.

Amesema yaliyojitokeza yanasikitisha kwani katika kumtafuta mkandarasi huyo huko Uturuki, imegundulika kwamba huyu hana eneo lake la ujenzi wa meli.

Badala yake amekuwa akipata zabuni na wao ni madalali, wanachukua zabuni wanatafuta kampuni nyingine wanawapa kazi.

“Pia imegundulika mbali na maelezo kuwa  kampuni hii ina fedha zinazotosheleza, ilibainika kwamba uwezo wake wa kifedha ni mdogo mno kwa sababu mpaka timu inaondoka Uturuki wameshindwa kutoa statement ya fedha walizonazo.

“Lakini wasifu wake kampuni na uwezo wake katika ujenzi ni wa mashaka kwani haipo hata kwenye orodha ya wajenzi wa meli inayotolewa na Umoja wa wajenzi wa Meli nchini Uturuki. Hii kampuni haimo na hiyo ndiyo ilitudhibitishia kwamba hawa ni madalali.

“Pia haikuwa na wafanyakazi wenye sifa za ujenzi wa meli na wala haina mitambo ya kujenga meli, hadi sasa haijafanya lolote kwenye kazi hii ambayo tulisaini nayo mwezi Juni mwaka huu,” amesema.

Amesema eneo ambalo walilitumia ni kampuni nyingine ya Kituruki ambayo hata hiyo yenyewe ilipokaguliwa ilibainika kuwa ina uwezo wa kufanya matengenezo ya meli na kutengeneza boti ndogondogo.

“Lakini ndugu zangu tujiulize tenda hii ilipotoka, ilitolewa na Bodi ya tenda ya wizara husika au shirika husika… shirika lile lina bodi ya wakurugenzi ambao wamepitisha tenda hii.

“Lakini pia nisema nina taarifa kwamba hata huyu mkandarasi alifanyiwa (due diligence) tathmini ya kina, ambayo ilisema yupo positive lakini timu iipokwenda yaliyobainika ni hayo.

“Sasa hayo tumebaini hivi karibuni, huko nyuma yametokea mangapi,? waziri na hili nalo ni mzigo wako naomba tena bodi ya wakurugenzi, jiulize tena hawa watu, hivi vikundi viwili bado wanakaa kwenye shirika kama miradi ilikuwa ni ya aina hii,” amesema.

Amesema amemuagiza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesas Makame Mbarawa achukue hatua ya kusimamisha hiyo tenda akishirikiana na mwanasheria mkuu wa Serikali ili kunusuru fedha zetu zisiliwe na wajanja wachache.

“Lakini cha kusikitishwa ni kwamba mwananchi wa ndani anashirikiana na nje kuchepusha fedha zote hizi ambazo zingekwenda kwenye kutekeleza maendeleo ya wananchi wanyonge kule chini, tuna uhaba wa madarasa, pembejeo za kilimo.

“Lakini huku kuna watu wamekalia fedha wanapitisha miradiu wanavyotaka, wanazitumia wanavyotaka. Tenda committee Bodi zipo mambo ni kama hayo.

“Naomba waziri fanya marekebisho kama unavyoweza kwenye wizara yako kama huwezi njoo tukae kitako mimi, wewe, katibu mkuu kiongozi, tuone jinsi ya kufanya marekebisho kwenye wizara hii ili mambo yaendelee

“Lakini fedha zinatumika hivyo, papo hapo kukiwa na wafanyakazi tele wa ngazi za chini ambao masilahi yao na stahiki zao pengine hawapewi kwa wakati au yapo chini. . ,” amesema.

Amsema yamkini wafanyakazi hao wangepewa fedha hiyo wangepata motisha ya kufanya kazi zaidi, kuliko kuwavuta kama wanavyowavuta sasa.

“Waziri wa Ujenzi (Prof. Mbarawa) nilikuweka kwa kukuamini naomba nenda kasimamie kazi hii kama ninavyotarajia na utakaposhindwa niambie dada nimeshindwa! nitaangalia mwingine atakayenisaidia. Lakini haya hayawezi kuendelea,” amesema.

Kutokana na hali hiyo Rais Samia ametangaza kuvunja Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), sambamba na kutengua uteuzi wa wenyeviti wa bodi hizo.

“Kwa hiyo wenyeviti wote wawili nadhani bodi ya shirika la meli sijui kama niliunda upya au vipi … wenyekiti wote wawili wa bodi nimewaondoa.

“Waziri utafanya palipobakia, tena bodi hizo si uwezo wangu ni uwezo wako na watu wako, nasubiri nione kitakachotokea. Hatuwezi kuendelea na mambo ha

ya alafu mnachukua malawama mnatupia kusikohusika, haiwezekani!” amesema Rais Samia

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!