Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uhuru wa kisiasa: JPM atoa neno zito
Habari za Siasa

Uhuru wa kisiasa: JPM atoa neno zito

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) amesema, uhuru wa kisiasa hauna maana kama nchi za Afrika zitaendelea kuwa tegemezi kiuchumi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Novemba 2019, wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na NORDIC, jijini Dar es Salaam.

“Viongozi wengi wa Afrika tumetambua kuwa, mustakabali wa Bara letu uko mikononi mwetu, na kwamba uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa wa maana sana, endapo mataifa yetu yataendelea kuwa tegemezi kiuchumi,” amesema Rais Magufuli.

Na kwamba, mataifa ya Afrika hayawezi kuwa Huru wa kujiamulia masuala yake, iwapo yataendelea kuwa ombaomba. Na kuwa, viongozi wa Bara hilo jukumu lao ni kutafuta ukombozi wa kiuchumi.

“Hatuwezi kuwa na Uhuru wa kujiamulia mambo yetu wenyewe, endapo mataifa yetu yataendelea kuwa ombaomba. Kutafuta ukombozi wa kiuchumi ndio jukumu la viongozi wa Afrika. Hata Mwalimu Julius Nyerere alisema, ukombozi wa Afrika ni kujikomboa kiuchumi,” amesema Rais Magufuli.

Pia, amesema ushirikiano wa kutoa na kupokea misaada, hauhitajiki kwa sasa, kwani sio endelevu.

“Pamoja na uhusiano mzuri na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye ushirikiano, bado tuna fursa ya kukuza ushirikiano wetu ili kuleta manufaa kwa pande zote mbili.

“Na suala  hili ni muhimu kwasababu, kwa muda mrefu ushirikiano wetu umejikita zaidi kwenye kutoa na kupokea misaada, ushirikiano wa aina hii sio endelevu na wala hauhitajiki katika mazingira ya sasa, “ amesema Rais Magufuli.

Kiongozi huyo wa Tanzania amependekeza nchi za Afrika kubadilisha ushirikiano, kutoka kwenye ushirikiano wa kupokea misaada, kwenda kwenye ushirikiano wa kiuchumi.

“Ni lazima tubadilishe muelekeo na kuingia kwenye uhusiano wa kisasa baina ya mataifa, ambao unajikita kwenye uchumi kupitia biashara na uwekezaji.  Diplomasia ya uchumi ndio iwe kwenye ushirikiano kwa mataifa yetu,” ameeleza Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!