Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo kuifuata Chadema?
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo kuifuata Chadema?

Spread the love

UKAKASI, hujuma na mbinu chafu zinazofanywa na wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa, zinaelekea kuvuruga maana ya uchaguzi huo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Chama cha ACT – Wazalendo, leo mchana tarehe 8 Novemba 2019, kinatarajia kufanya uamuzi wake, kuhusu hujuma zilizofanywa na wasimamizi hao kwa kuengua wagombea wake.

Mpaka sasa, taarifa zinaeleza kuwa jumla ya wagombea 110,040 wa chama hicho, wameenguli kwa madai mbalimbali ikiwemo kujaza fomu ndivyo sivyo.

“Leo viongozi wakuu wa chama watakutana na kufanya uamuzi mkubwa, mkutano unaratajiwa kuanza mchanga na kumalizika usiku,” amesema Ado Shaibu, katibu mwenezi wa chama hicho.

Wakati viongozi wakuu wa chama hicho wanakutana leo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), tayari kimefanya uamuzi wa kutoshiriki uchaguzi huo.

“”Hatuwezi kuwalaumu watendaji kwa kuwafanyia mizengwe wagombea wetu, hatuamini kama watendaji wanaweza kufanya figisu hizo viongozi wa serikali wasijue, Waziri Mkuu asijue, wala Jafo asijue!

“Hii ni hujuma na ni unafiki na sasa hii ijulikane kuwa CCM na serikali kwa ujumla wake ni waoga, haiwezekani wakawa wanajigamba kununua ndege, ujenzi wa barabara na miradi mbalimbali ya maji wakati huo wanaogopa uchaguzi,” alisema Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema – Taifa.

Mbowe ametoa mfano kwamba, katika jiji la Dar es Salaam, chama Chadema kilikuwa na jumla ya wagombea 570 lakini waliopitisha kugombea ni 26 pekee.

Awali, Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dorothy Semu, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, alidai kuenguliwa kwa wagombea wao, kulipangwa mapema ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa.

“Wagombea wetu 110,040 nchi nzima wameenguliwa, wakiwamo 2,000 ambao hata sababu za kuenguliwa kwao hazijaelezwa.

“Kuenguliwa kwa wagombea hawa na wengine kutoka vyama vya upinzani kumelenga kuhakikisha wagombea wa CCM wanapita bila kupingwa,” alisema Semu.

Seleman Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tamisemi amesema, uamuzi wa Chadema kugomea uchaguzi licha ya kuwa haki yao, kunanyima fursa wagombea wa chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!