Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vyama 11 kushiriki uchaguzi, Zitto ahoji walipo wagombea wao
Habari za SiasaTangulizi

Vyama 11 kushiriki uchaguzi, Zitto ahoji walipo wagombea wao

Viongozi wa Vyama vya Siasa 11 visivyokuwa na uwakilishi bungeni wakitoa msimamo wao
Spread the love

VYAMA vya Siasa 11 visivyokuwa na uwakilishi bungeni, vimetangaza kushiriki uchaguzi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Vyama hivyo ni Sauti ya Umma (SAU), NRA, ADC, UDP, UMD, CCK, ADA- TADEA, Demokrasia Makini, TLP na AAFP.

Uamuzi huo umetangazwa leo tarehe 8 Novemba 2019 na Adbul Mluya, kiongozi wa vyama hivyo, wakati akizungumza na wanahabari.

Mluya ameeleza kuwa, vyama hivyo vinaimani kwamba, wagombea wake walioenguliwa katika zoezi la uteuzi wa kugombea uchaguzi huo, watarudishwa na Wizara Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

“Tutashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, huku tukiwa na imani kubwa wagombea wote waliotaka kushiriki TAMISEMI itawarudisha,” amesema Mluya.

Hata hivyo, Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amehoji kwenye mtandao wake wa twitter kwamba, vyama hivyo vimesimamisha wagombea sehemu gani.

“Wameweka wagombea wapi? Kama 90% ya nafasi CCM wameshatangazwa kupita bila kupingwa, wao wanashiriki uchaguzi gani?” ameandika Zitto, Mbunge wa Kigoma Mjini.

Uchaguzi huo tayari umesusiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na rafu zinazofanywa kupitia wasimamizi wa uchaguzi huo.

ACT-Wazalendo, baadaye leo tarehe 8 Novemba 2019, viongozi wakuu wanatarajiwa kukutana na kuja na msimamo mmoja kuhusu kushiriki uchaguzi huo.

Taarifa mpya iliyowekwa kwenye ukuraswa wa twitter wa ACT-Wazalendo imeeleza, kwamba;-

“Wagombea wote walikuwa 173,593, Uenyekiti wa Mitaa 2,481, wenyeviti wa Vijiji 8,218, Vitongoji 35,457,  wagombea wa nafasi za ujumbe wa Halmashauri za Vijiji na Kamati za Mtaa walikuwa 135,675. Wamebakizwa 4% ya wagombea wote tulioweka. 166,649 wameondolewa.

Hata hivyo, vyama hivyo visivyo na wagombea kupitia Mluya vimeeleza, haviwezi kuususia uchaguzi huo, kwa maelezo kwamba vinataka kupata mtaji wa kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

“Tutaendelea na uchaguzi kwa sababu siku zote anayesusa chakula ni yule aliyeshiba, mwenye njaa hawezi kususa, ana wabunge, madiwani halafu hashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa haathiriki.

“Mimi ninataka nipate mtaji niende serikali za mitaa, nikashinde nipate mbunge, unasusa kwa hoja ipi?” amehoji Mluya.

Miongoni mwa hujuma zilizotajwa na Chadema pamoja na vyama vingine vya upinzani, ni kuenguliwa kwa wagombea wake katika mchakato wa uteuzi wa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, kinyume na sheria.

Hata hivyo, vyama hivyo 11 visivyokuwa na uwakilishi bungeni, havikuwahi kuibuka mbele ya umma na kuilalamikia changamoto hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!